27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

R. Kelly aomba kutoka jela, kisa Corona

CHICAGO, MAREKANI

STAA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Robert Kelly, maarufu kwa jina la R. Kelly, amemuomba jaji kumtoa katika gereza la Chicago Metropolitan Correctional Center kutokana na kuhofia kuenea kwa virusi vya Corona.

Virusi vya Corona kwa sasa nchini Marekani vinaathiri kwa kiasi kikubwa jambo ambalo limesababisha idadi kubwa ya wafungwa kuachiwa huru.

Virusi hivyo vimekuwa vikienea hasa kwenye mkusanyiko wa watu pale ambapo wanagusana, hivyo wafungwa ni rahisi kupata kutokana na mrundikano, hivyo msanii huyo ameomba kuachiwa huru kama ilivyo kwa wafungwa wengine.

Msanii huyo amewekwa ndani kutokana na kashfa ya unyanyasaji wa kijinsia ambapo kuna uwezekano wa kukaa jela zaidi ya miaka 10.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles