28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

QNET ilivyookoa vijana wasio na ajira, kipato kidogo

MWANDISHI WETU

MAUZO ya moja kwa moja, (network marketing) yamekua kwa kasi katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika na hasa Afrika Mashariki.

Kukua huku kwa kiasi kikubwa kumesababishwa na ongezeko la idadi ya watu wakiwamo vijana mahiri.

Kwa mujibu wa taarifa ya Uchambuzi wa Ongezeko la Vijana ya Taasisi ya Maendeleo ya Afrika, Afrika Mashariki ina zaidi ya asilimia 45 ya vijana kati ya watu milioni 150 walioko Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda. 

Vijana hawa wengi wana elimu, kwa ujumla wana ufahamu wa teknolojia, wepesi kufuata mienendo mipya, wana hamasa ya kuweka juhudi na fikra za ujasiriamali – jambo ambalo ndio sifa ya awali ya mafanikio endelevu katika biashara ya uuzaji wa moja kwa moja.  

Kwa wanaoanza, mauzo ya moja kwa moja ni wazo la biashara ya kimataifa na linaelezewa kama ‘uuzaji wa bidhaa za matumizi au huduma, kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, mbali na maeneo ya maduka ya kawaida’.

Mtindo huu wa mauzo una zaidi ya miaka 100 sasa. Sasa hivi takribani watu milioni 117 wanajihusisha nayo.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2018 ya Shirikisho la Chama cha Wauzaji wa moja kwa moja Ulimwenguni. (World Federation of Direct Selling Association (WFDSA), mauzo ya moja kwa moja yalizalisha Dola za Marekani bilioni 190 na karibu nusu ya mauzo yote yametoka katika masoko yanayochipukia.

Inatosha kusema kwamba Afrika ina chukua chini ya asilimia moja ya jumla ya mauzo ya WFDSA, lakini wataalamu wanakadiria kwamba soko la Afrika Mashariki linatoa fursa ya kukua kwa wajasiriamali wanaochipukia na hata kwa wale walioajiriwa na wana kiu ya kujipatia kipato cha nyongeza kupitia mauzo ya moja kwa moja.

Katika kanda ambayo mahitaji ya ajira rasmi yanazidi kuwa na ushindani mkubwa na uhaba wa ajira rasmi, mauzo ya moja kwa moja yanatoa njia mbadala za ajira tofauti na ilivyozoeleka kwa wale wanaohitaji kipato cha ziada au mazingira hayaruhusu ajira.

Akizungumza na waandish wa habari hivi majuzi, Meneja Mkuu wa QNET kwa kanda ya kusini mwa Jangwa la Sahara, Biram Fall, anasema: “QNET imesaidia kuwawezesha maelfu ya watu Afrika, hasa vijana, katika muongo uliopita.

“Tunaona ongezeko la kukubalika kwa mauzo ya moja kwa moja, na idadi ya watu zaidi ya milioni 200 katika Afrika Mashariki, mtindo huu  unabadilisha maisha ya wengi.”

Anasema QNET inatoa aina mbalimbali za bidhaa za afya, ustawi na mitindo ya maisha kupitia mifumo yake ya biashara ya mitandao (e-commerce) kwa mamilioni ya wateja katika zaidi ya nchi 100, ikiwa inasaidia watu kuishi maisha bora na kutoa njia mbadala ya kujipatia kipato kwa yeyote anayehitaji kutumia fursa hii.

Fall anasema kampuni pia ina ofisi na mawakala washirika katika nchi 25 duniani kote, pia ina stoo zaidi ya 50, shughuli za uendeshaji, maduka na wauzaji katika nchi kadhaa duniani.

“Uwepo wake imara katika Afrika Mashariki, QNET imejidhatiti katika kuendeleza mtindo wa mauzo wa moja kwa moja katika kanda hii.

“Pia inarudisha faida yake kwa jamii. Baadhi ya wanufaika wa majukumu ya kampuni kwa jamii ni pamoja na kituo cha kulelea yatima cha Maunga, Newlife Orphans Home ambavyo vimepokea msaada wa chakula na michango kwa miaka ya hivi karibuni.” 

Kwa mujibu wa Fall QNET ina nia ya kurudisha kwa jamii, hii ndio sababu kwanini wamewekeza kwa kiasi kikubwa katika miradi ya uwajibikaji endelevu ya kampuni kwa jamii katika maeneo mbalimbali ya Afrika kupitia mkono wao wa uwajibikaji kwa jamii.

Anasema QNET Ghana, kwa kupitia RYTHM Foundation, imetoa vifaa maalumu 50 vya kusomea vitabu vya kielektroniki (Kindle e-readers) ambavyo vina vitabu 100 vinavyoendana na tamaduni zao kila kimoja.

Vitabu hivyo ni kwa ajili ya wanafunzi wa Nima, eneo lenye watu wa kipato cha chini zaidi ndani ya Jiji la Accra, Ghana. 

Anasema ulikuwa ni mradi uliofanyika kwa ushirikiano na Worldreader, NGO ya  utoaji wa elimu duniani na Achievers Ghana, taasisi ya elimu kwa jamii.

QNET pia inafanya vizuri katika udhamini wa michezo duniani. Baadhi ya ushirikiano mkubwa wa hivi karibuni unajumuisha kuwa wauzaji wa moja kwa moja wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester City na Klabu ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake ya Manchester City na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa ajili ya ligi ya mabingwa ya Total CAF, Kombe la shirikisho la Total CAF na Total CAF Super Cup kwa mwaka 2018 na 2019. “Hapo awali washirika wakubwa walikuwa ni pamoja na Formula One, badminton na zaidi, kutokana na imani thabiti ya kampuni kwamba msukumo, shauku na kufanya kazi katika timu iliyopo katika michezo inaendana na ule wa QNET,” anasema Fall.

Manufaa

Anaongeza: “QNET inaamini kwamba hakuna kinachowezesha zaidi kwa mtu binafsi kama uhuru wa kifedha ambao unatolewa na jitihada katika sekta ya mauzo ya moja kwa moja. Pia inaamini kwamba watu wa Afrika Mashariki, pamoja na shauku yao na fikra za ujasiriamali, watafurahia kiwango bora cha bidhaa zinazotolewa na QNET na fursa za kibiashara kwaajili ya maendeleo binafsi.

“Mauzo ya moja kwa moja yanaweza kuwa ni kazi ya kutosheleza kwa wale wanaochagua kuchukua fursa hii kama kazi yao kuu au hata kuchukua kama kazi ya ziada kwa sababu inatoa faida za kifedha kutegemeana na muda na juhudi unazoweka katika kukuza biashara yako.”  Anasema tofauti na biashara zingine za kawaida ambazo zinahitaji mtaji mkubwa, rasilimali na hata uzoefu, biashara ya mauzo ya moja kwa moja inatoa fursa hii ya biashara yenye gharama nafuu kwa kila mmoja anayehitaji kuianzisha, bila kujali kiwango chao cha elimu au uzoefu.

Zaidi ya hayo, anasema mafunzo na maelekezo ambayo wafanyabiashara wanaoanza wanapitia (Wawakilishi wa Kujitegemea au IRs kama ilivyo katika QNET) inawapatia ujuzi wa pekee ambao unawasaidia kuwa na ujasiri, kujitambua na hatimaye ukuaji binafsi ambao unatambua utaalamu wa mtu kama mjasiriamali aliyekamilika.  

“Huenda, manufaa makubwa zaidi ya mauzo ya moja kwa moja katika masoko yanayoibukia kama Afrika Mashariki ni kwamba mtindo huu unakuwa na athari zaidi hapa kuliko katika masoko yaliyoendelea kwa sababu ya athari za kifedha inayoweza kuleta katika maisha ya watu – kutoa fursa za ujasiriamali kwa wote, bila kujali ujuzi au uzoefu, hivyo kuchangia kupunguza umasikini katika jamii,” anasema na kuongeza: 

“Katika mizizi ya QNET, kuna falsafa ya RYTHM – Raise Yourself To Help Mankind – ambayo inaongoza jitihada zake zote, na kuendesha kampuni si tu kubadilisha maisha ya watu duniani kote, lakini pia kushirikiana nao katika kupanua athari hizi.” 

Kama alivyosema bwana Trevor Kuna, Mkurugenzi Mtendaji wa QNET  “Tunaamini kwamba mafanikio ya kifedha peke yake hayatoshelezi, ili tuweze kuleta athari, tunahitaji kuendeleza watu kuwa binadamu bora ili waweze kutumia mafanikio yao kuchangia katika jamii.”

Changamoto

Kama ilivyo katika biashara nyingine yoyote, sekta ya mauzo ya moja kwa moja pia inakabiliana na changamoto.

Anataja changamoto ambayo ni kubwa zaidi ni kuenea kwa mifumo ya pyramid schemes inayoenda kinyume cha sheria ambayo inaonekana kama kampuni halisi za biashara ya moja kwa moja, ikiwa inaahidi wawekezaji kuwa watajipatia faida nyingi kupita kiasi iwapo wataunganisha watu wengine.

“Ukweli ni kwamba hawa ni ‘matapeli’ wanatengeneza taswira potofu ya sekta ya mauzo ya moja kwa moja, jambo ambalo linatengeneza kikwazo kwa kampuni halisi kama QNET kusajili washauri wa kibiashara kuendesha biashara zao halisi na halali,” anasema.

Anataja changamoto nyingine kuwa ni ujuzi ambao haujaendelezwa hasa kwa wale ambao wamechukua fursa hii hivi karibuni.  QNET inasema, inatatua changamoto kwa kuweka msisitizo mkubwa katika mafunzo na elimu kwa IRs.

Mafunzo hayo si tu kwamba yanaendeleza ujuzi wao wa kitaalamu, lakini pia unalenga katika ukuaji na maendeleo binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles