24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Q BOY MSAFI AFURAHIA KUWAVALISHA P SQUARE, DAVIDO

Na CHRISTOPHER MSEKENA-DAR ES SALAAM

MWANAMITINDO na msanii wa Bongo Fleva, Siras Chassama ‘Q Boy Msafi’ ambaye aliwahi kuwa msimamizi wa mwonekano wa staa wa muziki nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, amesema tayari amewahi kuwavisha mastaa wakubwa barani Afrika.

Akizungumza na MTANZANIA, Q Boy ambaye hivi sasa anasimamia mwonekano wa msanii Young Dee, alisema kwa hapa nyumbani tayari amewahi kuwavisha wasanii kama Shetta, Harmonize, Rich Mavoko na wengine wengi.

“Mbali na Diamond Platnumz, najivunia kufanya kazi na wasanii wakubwa Afrika, nimewahi kuwavisha P Square na Davido kipindi kile alipokuja Bongo, kwani ni hatua kubwa ambayo haiwezi kufutika kwenye historia yangu,” alisema Q Boy Msafi anayefanya vyema na wimbo wake, Karorero.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles