21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

PUSHA T, VIRGINIA WAFUNGA NDOA

NEW YORK, MAREKANI


Hatimaye staa wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Terrence LeVarr Thornton maarufu kwa jina la Pusha T, amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Virginia Willams.

Ndoa hiyo imefungwa kwenye Hoteli ya Cavalier Beach, huku mastaa mbalimbali wakihudhuria kama vile Kim Kardashia, Kanye West, Trey Songz, Pharrell Williams ambaye alikuwa kama Best Man wa Pusha T na wengine wengi.

Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aliwashukuru mashabiki zake ambao walimtumia ujumbe mbalimbali kwa ajili ya kumtakia kila la heri katika maisha yake mapya ya ndoa.

“Ni ukurasa mpya wa maisha yangu, nimeamua kufunga ndoa na Virginia ambaye nimekuwa naye pamoja kwa kipindi kirefu, nawashukuru mashabiki kwa sapoti yenu katika kipindi hiki chote,” aliandika rapa huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles