25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Puma yazindua mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Mafuta ya Puma, imezindua mafunzo na uchoraji la usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi ambayo yatawapa uelewa kwa usalama.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Puma, Dominic Dhanah, amesema lengo la kuwahusisha wanafunzi wa shule za msingi ni kutokana na imani yao kwamba watoto hao wanahitaji mafunzo ya usalama barabarani ili kuepukana na ajali.

“Watoto hawa wanakabiliwa na hatari ya ajali za barabarani hivyo wanahitaji mafunzo ya usalama barabarani kitu ambacho ni kipaumbele namba moja kwa Puma na tumeamua kuwafundisha watoto wadogo kwani tunfahamu hatari za barabarani wanazokabiliana nazo.

“Kampuni ya Puma inafanya biashara ya mafuta katika nchi 49 duniani na kwa Afrika tupo katika nchi 19. Mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi yalianza mwaka 2013 hapa Tanzania na hadi sasa shule 75 zimenufaika na mafunzo haya wakati wanafunzi 80,000 wamepata mafunzo haya.

“Tumefanya utafiti na kugundua kuwa shule tulizoendesha mafunzo haya, ajali kwa wanafunzi zimepungua na hivyo basi kwa mwaka huu mafunzo haya yataendeshwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar,” amesema Dhanah.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Yussuf Masauni, amesema Serikali inafarijika na kazi inayofanywa na Kampuni ya Puma kwa kurudisha faida inayopatikana kwa jamii ikiwamo kutoa mafunzo muhimu ya usalama barabarani.

“Elimu ni suala la kipaumbele kwa jamii na mkakati wetu ni kupunguza ajali za usalama barabarani na Puma inafanya kazi hii kwa karibu na Machi 30, mwaka huu tutakuwa na kongamano la wiki ya usalama barabarani pia tujadili hili kwa kina,” amesema Masauni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,763FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles