23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

PSPTB yawahimiza waajiri kutuma taarifa za watumishi wa kada hiyo

Na FARAJA MASINDE

WAAJIRI wote nchini wametakiwa kutuma taarifa za Watumishi wa kada ya ununuzi na Ugavi ikihusisha pia katika Kitengo, idara  hiyo, vyeo vyao, hali ya usajili, ukubwa wa manunuzi katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Agizo hilo limetolewa leo Jumanne Desemba 17, 2019 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurungezi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi, ambapo amesema kuwa taarifa hizo zitahusisha utendaji wao ili kuwezesha bodi hiyo kufanya thathimini.

“Lengo la kuwaagiza waajiri wote nchini kutuma taarifa hizo nikutaka kuiwezesha bodi kufanya tathimini ya uwezo na uhitaji wa wataalamu katika fani husika.

“Na tayari katika kulufanikisha hili, Oktoba mwaka huu bodi iliziandikia barua taasisi za umma 576 ikizitaka ziwasilishe taarifa za watumishi wote wanaofanyakazi za Ununuzi na Ugavi katika ofisi zao,” amesema Mbanyi.

Aidha, Mbanyi amesema kuwa, hadi sasa kati ya taasisi 460 zilizoandikiwa barua hiyo, bado hazijaleta taarifa husika na kusisitiza kuwa suala hilo linakwamisha bodi hiyo kutekeleza wajibu wake wa kisheria katika kupanga, kuelekeza na kuratibu mahitaji ya wataalamu wa fani hiyo.

“Kwa mwenendo huu inakuwa ni ngumu kuishauri Serikali mahitaji ya wataalamu katika taasisi za Umma, hivyo (PSPTB) inatoa wito kwa wakuu wa taasisi na waajiri nchini kuleta taarifa za watumishi wanaofanya kazi za ununuzi na ugavi kabla ya Januari 31, mwakani.

“Pia bodi inatoa wito kwa Watalaamu wa Ununuzi na Ugavi kufanya kazi kwa weledi, umakini na bila kuwa na hofu ili kupata thamani ya fedha kwenye manunuzi wanayofanya kwa ajali ya manufaa ya taifa,” amesema Mbanyi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles