Na Mwandishi Wetu,Mtanzania Digital
Kampuni ya Smartfoundry imezindua programu yake tumishi(APP) ya ‘Rifaly’ ambayo ni maboresho ya bidhaa ya ‘M-Paper’ yenye makao makuu yake Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mtanzania Digital, Mkuu wa Smart Foundry, Johnnes Lutainulwa amesema Programu ya Rifaly itwawezesha watu kupata mahudhui ya magazeti, majarida, vitabu, nakala na hadithi za sauti lengo likiwa ni kufungua ulimwengu kwa Watanzania kupitia mfumo huo ili kuwezesha kukuza soko la ubunifu wa maudhui kupitia mfumo huu mpya wa ‘RIFALY’.
Lutainulwa ameongeza kuwa vijana wengi wamejikita kwenye ubunifu wa maudhui ila wamekuwa wakipata tabu kwa kuwa mifumo iliyopo siyo rafiki kwao, hivyo kutumia mfumo weo wa ‘RIFALY’utaweza kuleta tija kwa watanzania.
”Tumeona vijana wamejikita kwenye ubunifu wa maudhui na mifumo iliyokuwepo tunahisi si rafiki kwao sababu siyo mifumo ya nchi hii hivyo sisi tunaamini tunaweza tukawasaidia vijana waweze kutengeneza kipato tofauti tofauti kwenye upande wa ubunifu wa maudhui,”amesema Lutainulwa.
Kwa upande wake, Fredrick Bundala wa Simulizi na Sauti amefurahishwa kwa maboresho hayo ya M-paper kwani kumesaidia kuongeza wigo kwa wabunifu wa maudhui hasa kwa njia ya sauti maarufu kama ‘podcast’ hivyo kutawawezesha wabunifu mbalimbali kuweka kazi zao hasa waandishi ili kuweza kuwaongezea kipato.