28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Programu tano za kilimo kuzinduliwa Nanenane Simiyu

Derick Milton-Simiyu.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, amesema jumla ya programu tano za kimkakati za kuboresha sekta ya kilimo na mazao yake zitazinduliwa rasmi wakati wa maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) kitaifa zinazofanyikia viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Amesema hayo leo Jumanne Julai 30, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja hivyo mara baada ya kukagua maandalizi ya maonesho hayo, ambapo amesema serikali imedhamiria kuifanya sekta ya kilimo kuwa mkombozi wa uchumi wa nchi.

Hasunga amesema kuwa programu hizo zitazinduliwa na viongozi wakuu wa kitaifa, wakiwemo Rais John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambapo kati ya programu hizo ni mfumo wakudhibiti upotevu wa mazao ya wakulima.

Programu nyingine ni Bima ya mazao ambayo nayo itazinduliwa ikiwa na lengo la kuwasaidia wakulima na wawekezaji kwenye kilimo endapo watapata hasara kwa mazao yao kukubwa na mafuriko, ukame, na magonjwa.

Aidha amesema programu nyingine ni uzinduzi wa mfumo wa soko la bidhaa, ambao utakuwa wa kieletroniki ambao utatusaidia kupata masoko na kuuza mazao yetu kwenye soko la dunia, pamoja na kuzinduliwa mfumo mwingine wa tatu wa kieletroniki unaolenga kuboresha biashara ya mazao ya wakulima.

“Mfumo huu wa kieletroniki wa tatu umelenga kuondoa vikwazo kwa wafanyabishara ambao wanauza mazao yetu nje ya nchi katika kupata vibali na leseni, tunataka sehemu popote walipo waweze kupata vibali hivi kwa njia ya mtandao,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles