28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA MBARAWA ATEMBELEA MRADI WA UCHIMBAJI VISIMA VIREFU

Na Mwandishi wetu      |     


WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa leo ametembelea mradi wa uchimbaji visima virefu vya Kimbiji na Mpera unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam  (Dawasa).

Ziara hiyo ya ni muendelezo wa kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Dawasa.

Visima vya Kimbiji na Mpera ni moja ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na wizara hiyo kwa lengo la kuongeza wingi wa maji katika eneo la huduma ya Dawasa kutoka lita milion 300 mpaka lita 720 zitakazotoshereza eneo hilo hadi mwaka 2032.

Visima hivyo vina kina kati ya mita 435 na 625 huku baadhi vikiwa na uwezo wa kuzalisha maji kati ya lita 100,000 hadi 450,000 kwa saa.

Kwa jumla visima vyote vinatarajiwa kuzalisha maji lita milioni 260 kwa siku.

Tayari visima 19 kati ya 20 vimechimbwa kwa urefu tofauti.

Mradi huo unatekelezwa na mkandarasi NSPT ya Iran na Serengeti ya Tanzania kwa gharama ya Sh Bilion 19.8.

Kukamilika kwa mradi huu kutaimarisha upatikanaji wa maji katika maeneo ambayo hayakuwa na huduma nzuri ya maji na maeneo yasiyokuwa na mtandao rasmi.

Maeneo hayo ni pamoja na Kigamboni, Kibada, Kisarawe II, Kongowe, Segerea, Gongo la mboto, Pugu ,Chanika, Chamazi, Charambe, Buyuni, Mbagala na Makangarawe.

Maeneo mengine ni Tazara, Ukonga, eneo la viwanda la Barabara ya Nyerere, Uwanja wa ndege, Kiwalani, mji wa Mkuranga, mkoani Pwani pamoja na vitongoji vyake vikiwamo Kisemvule na Kibamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles