24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA MBARAWA AIOMBA AFDB KUIUNGA MKONO TANZANIA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ameiomba Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika mkakati wake wa kukuza uchumi kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu.

Akizungumza na wakurugenzi wa Bodi hiyo waliomtembelea ofisini kwake Dar es Salaam jana, Profesa Mbarawa aliishukuru benki hiyo kwa ushirikiano inaoipa Serikali ya Tanzania katika miradi mingi ya ujenzi wa barabara na kuiomba kuiunga mkono katika uwekezaji mkubwa inaoufanya katika miradi ya usafiri wa anga na reli.

“Tumejipanga kukuza uchumi kwa kuimarisha sekta za barabara, anga, reli na bandari, hivyo tunaomba ushirikiano wenu kadri tunavyouhitaji ili kufikia malengo yetu kwa wakati,” alisema.

Aidha, Waziri Mbarawa aliitaja baadhi ya miradi ya barabara ambayo Tanzania imenufaika kutokana na AfDB kuwa ni barabara ya Kibondo-Kasulu-Manyovu (km 250), Makutano-Nata-Mugumu-Mto wa Mbu hadi Loliondo (km 213), Makurunge-Saadani-Pangani-Tanga (km 178) na barabara za pete jijini Dar es Salaam (km 34).

“Kuimarika kwa sekta ya miundombinu nchini, hasa sekta ya anga, reli na barabara, kutaimarisha sekta za utalii na kilimo na hivyo kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa,” alisisitiza.

Kwa upande wake, mjumbe wa Bodi ya AfDB, Dk Weggoro Calleb, akizungumzia umuhimu wa miradi ya ujenzi inayoanzishwa hapa nchini, alisema imeweza kutoa fursa za ajira kwa wananchi na kuwekewa mazingira endelevu ili ilete mabadiliko chanya katika maisha ya watu na taifa kwa ujumla.

Aidha, bosi huyo wa AfDB alisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika ujenzi wa miundombinu ili kuiwezesha nchi kuwa na miundombinu bora na ya kutosha na hivyo kuchochea maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles