30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Lipumba kuanza ziara mikoani

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba

* Kutua mikoa ya Lindi, Mtwara na Tanga

HADIA KHAMIS Na PATRICIA KIMELEMETA, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba, leo anatarajiwa kuanza ziara katika mikoa mbalimbali.

Katika ziara hiyo Profesa Lipumba ataandamana na viongozi watano waliosimamishwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi, ambapo pamoja na mambo mengine atafanya vikao vya ndani na wanachama na viongozi wa ngazi za wilaya kueleza kiini cha mgogoro uliopo ndani ya CUF.

Profesa Lipumba atafanya ziara hiyo katika mikoa mitatu ya Lindi, Mtwara na Tanga huku Jumuiya ya Vijana ya chama hicho, (JUVICUF), ikiwataka wanachama na viongozi kutompa ushirikiano kiongozi huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Hamidu Bobali,  alisema hatua ya kufanyika kwa ziara kwa kiongozi huyo kutaendeleza chuki ndani ya chama hicho.

“Nawaomba wanachi wote wa kusini kutotoa ushirikiano kwa viongozi hao kwa sababu lengo lao kwa sasa ni kutaka kukivuruga chama kwa sababu chama kipo salama,”alisema Bobali ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi.

Alisema mgogoro uliopo CUF haumuhusishi Maalim Seif na Profesa Lipumba bali unawahusu watu na watu.

Pamoja na hali hiyo Bobali alisema kuwa JUVICUF, inaunga mkono maamuzi yote halali yaliyofanywa na Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho la kumfukuza na kuwasimamisha kazi baadhi ya wanachama akiwemo Profesa Lipumba.

“Inashangaza sana kila taasisi ina utaratibu wake lakini katika siku za hivi karibuni kumeibuka kikundi cha  wanachama wa CUF Mkoa wa Dar es Salaam na kuzungumza na vyombo vya habari kinyume cha utaratibu  wakati katiba ya chama haelezi kama kuna ngazi mkoa.

“Nawataka vijana wa CUF kuheshimu mamlaka za jumuiya ya vijana na kuwa na nidhamu ambayo wamelelewa nayo, kuliko kila mmoja kujifanya ana ndevu kama Kambare kwa kutoa kashfa dhidi ya viongozi,” alisema Bobali.

Akizungumzia hali ya kisiasa visiwani Zanzibar,  Bobali aliwataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu kwani tayari mikakati ya kurejesha tumaini la ushindi wao umeshaandaliwa.

Alisema mgogoro unaoendelea sasa hivi ni sehemu ya mikakati ya waliokuwa wasaliti katika chama hicho ili kuzima suala la Zanzibar.

Alisema licha ya taarifa kuzagaa kuwa Profesa Lipumba amefungua akaunti ili kuweza kuchukua fedha za ruzuku jambo hilo halitawezekana kwa sababu suala la kufungua akaunti linasimamiwa na bodi  ya wadhamini.

Kambaya afafanua

Akizungumza na MTANZANIA jana, Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhuano wa Umma, ambaye amesimamishwa uanachama, Abdul Kambaya, alisema ziara ya Profesa Lipumba mikoani imetokana na mwaliko alioupata kutoka kwa wanachama na wananchi wa mikoa ya kusini.

Alisema kitendo cha mwenyekiti wa Vijana wa JUVICUF kuzuia wananchi wasimpatie ushirikiano Profesa Lipumba  ni sawa na kulewa madaraka ya ujana kwani hana mamlaka hayo.

“Sisi hatubabaishwi na Bobali lazima tutafanya ziara kesho (leo)  kwa sababu yeye si msemaji wa wilaya na hii ziara Perofesa Lipumba amepewa mwaliko na viongozi na wanachama wa CUF,” alisema Kambaya.

Wakati huohuo upande wa uongozi wa CUF ambao unamuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, umesema unashangazwa  na kitendo cha Profesa Lipumba kufungua akaunti mpya ya chama kupitia Benki ya NMB tawi la Ilala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles