27.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Profesa Kamuzora aanza na utapiamlo Kagera

RENATHA KIPAKA, BUKOBA

KATIBU  Tawala wa Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora amesema pamoja na kuwa na majukumu mengi  ya kusimamia,  suala la utapiamulo ndani ya mkoa huo ni miongoni mwa  mambo hatarishi yanayopaswa kushughulikiwa  kuongeza uwezo wa kufikiri  watoto na kizazi kijacho.

Alitoa kauli hiyo juzi  alipokutana na watumishi wa ofisi yake ikiwa ni siku chache baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Alisema yuko mkoani humo kuleta mabadiliko ya  maendeleo,  uchumi,  afya na  fikra.

Profesa Kamuzora alitaja kipaumbele chake ni kuona namna bora ya kupambana na suala la utapiamlo hasa kwa watoto.

Alisema hiyo ni kwa kuzingatia  takwimu zunazoonyesha  Mkoa wa Kagera unashika nafasi ya nne kwa asilimia 41.7 kati ya mikoa 25 Tanzania Bara.

Alisema takwimu hizo zinatisha  na si rafiki katika ustawi wa jamii  kwa sababu  zinatengeneza  kizazi chenye  udumavu hasa wa akili  kwa watoto ambao ndiyo taifa la kesho.

“Kama hatutaangaika na suala hili la utapiamlo hatuwezi kusonga mbele kwa sababu hata uwezo wa kufikiri hasa kwa watoto wetu ni mdogo   utaendelea kuwa mdogo  jambo ambalo ni hatari kubwa kwa  vizazi vya sasa na vijavyo.

“Mkoa wa Kagera unakabiliwa na tatizo kubwa la utapiamlo ambako unashika nafasi ya nne kutoka mwisho ukiwa na asilimia 41.7.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,186FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles