22.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Profesa Kabudi: Tumeomba taasisi za kimataifa fedha kusamehe madeni

Mwandishi wetu -Dar e Salaam

SERIKALI imeziomba taasisi za fedha za kimataifa na nchi za Jumuiya ya madola kufikiria kufuta madeni yaliyokopeshwa kwa nchi zinazoendelea ili fedha hizo ziutumike kupambana na athari zilizotokana na Covid 19.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamamba Kabudi, aliyasema hayo alipomwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa marais, mawaziri wakuu na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Madola uliofanyika kwa njia ya mtandao (video conference) juzi katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Prof. Kabudi alisema katika mkutano huo, Tanzania imesisitiza tena umuhimu wa mashirika ya fedha ya kimataifa paoja na nchi za Jumuiya ya Madola zilizoikopesha Tanzania mbali na kutoa msamaha wa madeni, wafikirie kufuta madeni hayo ili kuziwezesha nchi zinazoendelea kuwa na fedha za kuboresha mifumo ya afya, na kupambana na athari zilizotokana na janga la Covid 19.

Katika mkutano huo, Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kati ya nchi za Jumuiya ya Madola na nchi zinazoendelea ili kuhakikisha kunakuwa na umoja na mshikamano katika kupambana na Covid 19.

“Mkutano huu umekuwa ni muhimu sana katika jumuiya yetu ya madola, tumesisitiza umuhimu wa kushirikiana, kuwa na misaada na mipango madhubuti ya mashirika ya kimataifa kuzisaidia nchi zinazoendelea katika jitihada zake za kuboresha na kujenga viwanda hasa vya kutengeneza dawa na vifaa tiba ili inapotokea majanga kama haya ya covid 19 ziweze kuwa na dawa na vifaa tiba kwa wananchi wake,” Amesema Prof. Kabudi

Alisema nchi nyingi mara baada ya janga la Covid 19 zilizuia utoaji wa dawa na vifaa tiba kwenda nje ya nchi kwa sababu dawa hizo walizihitaji kwa ajili ya matumizi yao wenyewe ndani ya nchi, ndiyo maana nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi Kusini mwa Afrika (Sadc) waliomba India kwa upendeleo kutupatia dawa na vifaa tiba vya kukabiliana na janga la corona.

Mkutano huo ulijadili pia umuhimu wa teknolojia katika kupambana na Covid 19 na kuboresha mifumo ya afya na kwamba wakati umefika teknolojia hiyo mahali popote ilipo ndani ya Jumiya ya Madola iweze kutolewa kwa nchi zote kwa gharama nafuu ili kuziwezesha nchi mbalimbali kutumia mifumo mipya ya kiteknolojia katika mifumo yake ya afya na kuziwezesha pia kupambana na Covid 19.

“Ni vizuri tuwe na mipango madhubuti na mikakati ya kupambana na aina hii ya majanga ambayo yanaweza kujitokeza siku za usoni na kufanya hivyo ni kuanza kujiandaa sasa kwa kuimaraisha huduma za afya katika nchi zetu,” alisema Prof. Kabudi.

Alisema  Tanzania imeanza jitihada hizo kwa kujenga hospitali nyingi za wilaya, mikoa pamoja na vituo mbalimbali vya afya na zahanati.

April, 2020 Rais Magufuli aliiomba Benki ya Dunia na mashirika ya fedha ya kimataifa kuzisamehe madeni nchi zinazoendelea ili nchi hizo ziweze kutumia fedha hizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID 19).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,429FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles