23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Kabudi awaonya wanaoisema Tanzania

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, amewataka watu wanaoisema vibaya Tanzania kukaa kimya kwa sasa.

Profesa Kabudi amesema hayo leo Jumatatu Februari 4, Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuapishwa kuwa waziri wa wizara hiyo na Rais John Magufuli aliyemteua juzi baada ya kufanya mabadiliko madogo ya mawaziri.

“Jana haikuwa siku nzuri kwangu niliamshwa na watu wengine kuambiwa kwamba nimeteliuwa katika nafasi hii, lakini nashukuru kwa kunipa nafasi.

“Huu si wakati wa kuisema nchi yetu, kuibeza na kuipagaza… nchi yetu ilijengwa na mwasisi Mwalimu Julius Nyerere, yeyote Mtanzania mwenye tatizo na nchi hii atutendee jambo moja tu, akae kimya.

“Tuna jambo moja tu kubwa la kujenga mahusiano na wale wanaoitakia mema nchi yetu,” amesema Profesa Kabudi.

Pamoja na Profesa Kabudi, pia Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Augustine Mahiga aliapishwa na baadhi ya Makamishna wa Jeshi la Polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles