33.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Prof. Ndalichako aipa jukumu bodi ya ufundi stadi

Na ASHA BANI -DAR ES SALAAM

WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameitaka Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  Stadi kusimamia majukumu ya VETA ili kuleta tija zaidi.

Profesa Ndalichako aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa bodi ya nane ikiwa ni pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri huku akiwataka kuendelea kusimamia vyema majukumu wanayopaswa kusimamia.

Aliyataja miongoni mwa majukumu hayo kuwa ni pamoja na kuongeza nafasi za utoaji mafunzo ya ufundi stadi kwa kujenga vyuo vipya, vikiwemo vya mikoa na wilaya.

A;itaja mafaniki hayo kuwa ni kuongeza karakana na madarasa, kuongeza mabweni ili kutoa nafasi zaidi kwa wanafunzi wanaotokea mbali na sehemu kilipo chuo, kukarabati miundombinu ya vyuo vikongwe vya VETA.

“Kuwaendeleza wafanyakazi wa VETA kitaaluma na umahiri kazini na kuwawekea wafanyakazi mazingira mazuri ya kazi ili kuongeza tija na uadilifu. Pamoja na utekelezaji wa majukumu mliyonayo kulingana na mpango mkakati wa VETA, napenda kuielekeza bodi hii ya nane kuzingatia miongozo ya Msajili wa Hazina katika utendaji wake wa kazi.

“… ikiwemo kuwasilisha taarifa za mahudhurio ya kila mwaka ya wajumbe wa Bodi kwa msajili wa Hazina ili kuona ni namna gani wajumbe wameshiriki kuisimamia Mamlaka kwa kipindi cha mwaka mzima,’’ alisema Prof. Ndalichako.

Pia aliwataka kuwasilisha taarifa ya maamuzi ya bodi kwa kila robo ya mwaka kwa msajili wa hazina ili kuifahamisha Serikali mwenendo na matarajio ya mamlaka na kujaza fomu za tathmini ya utendaji wa bodi kwa kila mjumbe na kufanya tathmini ya utendaji kazi wa kila mjumbe kwa kila mwaka ili kuweza kuzishauri mamlaka za uteuzi.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kujenga uchumi wa viwanda hivyo, wizara na taasisi zote zilizo chini yake, hazina budi kujitathmini ni kwa kiasi gani zitawezesha serikali kufikia azma hiyo Naye Mkurugenzi  Mkuu wa VETA, Dk. Pancras Bujulu alisema kuwa wamekuwa na mafaniko ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi wa kike kutoka asilimia 31 mwaka 2017 hadi asilimia 37 mwaka 2019.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles