24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mwakalila aleza mafanikio Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, umesema umepata mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali kwa kipindi cha miaka  mitano ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila alisema kipindi cha miaka mitano chuo kimepata mafanikio mengi, ikiwa ni pamoja na kuongeza udahili wa wanafunzi.

Alisema Kampasi ya Kivukoni, udahili umeongezeka kutoka wanafunzi 1,570 mwaka 2015 hadi 8,043 mwaka huu.

“Udahili huu pia umeongezeka Kampasi ya Karume-Zanzibar kutoka wanafunzi 22 mwaka 2015 hadi 1,753 mwaka jana.Idadi imeongezeka kutoka wanafunzi 1,592 wa mwaka 2014/15 hadi wanafunzi 9,799 mwaka 2019/20.

Alisema chuo kimeongeza idadi ya wahitimu,  ambapo Kampasi Kivukoni umeongezeka kutoka 569  mwaka wa masomo 2014/15 hadi wahitimu 3,237 mwaka wa masomo 2018/2019

Alisema  kipindi hicho,chuo kiomeongeza idadi ya watumishi kutoka 168 mwaka 2015, hadi watumishi 285 ambapo kati yao Kampasi va Kivukoni-Dare Salaam wapo 231 na Kampasi ya Karume, Zanzibar wapo 54.

“Chuo kiomeongeza idadi ya walimu na wahadhiri wenye shahada ya uzamivu(PhD) kutoka wahadhari wawili mwaka 2015 hadi 35 mwaka huu.

Alisema idadi ya programu za mafunzo ya kitaaluma, zimeongezeka  kutoka tatu za shahada zilizokuwepo mwaka 2015 hadi 10 na programu moja ya Shahada ya Umahili mwaka huu.

Alisema kipindi hicho,chuo kimeboresha mitaala yote, ikiwa ni pamoja na kuingiza somo la uongozi, maadili na uzalendo katika mitaala yote ili kila mwanafunzi awe na ufahamu wa kutosha juu ya uongozi, maadili na uzalendo.

 “Chuo kimekamilisha ujenzi wa ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 300 kwa pamoja na ofisi 10 za wafanyakazi, ujenzi ambao ulianza mwaka 2017 hadi mwaka jana.

Alisema  kimemaliza ujenzi wa hosteli za wanafunzi ambao ulisimama mwaka  2014 kwa sababu ya kukosa fedha za maendeleo.Alisema hoteli hiyo,ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 720.

 Kuhusu mazingira ya kufundishia, alisema wameboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi, ikiwa ni pamoja na uwekaji wa viti visivyo hamishika kwenye kumbi zote, ufungaji wa vifaa vya  kisasa katika kumbi za mihadhara, ununuzi wa kompyuta kwa ajili ya maabara za kompyuta.

Alisema chuo kimenunua magari manne, sita yakiwa mapya kwa ajiii ya kuwezesha utekelezaji wa majukumu mbalimbali.

Kuhusu changamoto ya mmomonyoko wa eneo la ufukwe wa Bahari, alisema wamefanikiwa kutatua tatizo  kwa msaada wa Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ilijenga ukuta.

“Chuo kimefanikiwa kutoa mafunzo ya muda mfupi ya uongozi, maadili, utawala bora, uzalendo kwa watendaji mbalimbali wa Serikali, wahitimu wanapewa mafunzo maalumu ya uongozi, maadili, uzalendo na utawala bora, zaidi ya wanafunzi 3,000 wamepata mafunzo haya,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles