24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mkenda aridhishwa Makumbusho ya Taifa

Na FERDNANDA MBAMILA

-DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda, ameridhishwa na uhifadhi na kazi iliyofanywa na Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Usalama wa Majengo ya Serikali ya kukiimarisha chumba maalumu cha urithi wa utamaduni na asili.   

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Profesa Mkenda alisema urithi huo wa utamaduni na asili ni pamoja na mafuvu na masalia ya binadamu wa kale.

Profesa Mkenda alisema Wizara ya Maliasili na Utalii itaimarisha sekta ya malikale na hususani Shirika la Makumbusho ya Taifa la Tanzania.  

“Wizara inaiimarisha na kuijengea uwezo Makumbusho ya Taifa ili itimize majukumu yake ya msingi ya kutafiti, kuhifadhi, kuonesha na kuelimisha umma juu ya urithi wa taifa na dunia kwa ujumla.

“Vitu hivi ni muhimu na ni urithi wetu, hivyo tunatakiwa kuvitunza kwa gharama yoyote kwani ni utambulisho wa taifa la Tanzania, vinaleta amani, mshikamano, uzalendo na furaha.  

“Aidha, vinavutia watalii wa ndani na nje na hivyo kuongeza pato la taifa,” alisema Profesa Mkenda.

Alisema matangazo kwenye luninga, redio na magazeti kuhusu vitu vinavyotunzwa Makumbusho ya Taifa, yatajenga uelewa kwa wananchi juu ya umuhimu wa makumbusho.

“Msipotangaza hakuna anayeweza kujua kuwa vitu muhimu kama hivi viko hapa Makumbusho ya Taifa, tunatakiwa tuwaambie wananchi ili waje kuviona,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles