30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mkenda ampa siku saba mrajisi wa vyama vya ushirika kutengua uamuzi

Na Upendo Mosha,Dodoma

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda, amempa siku saba Mrajisi wa Taifa wa Vyama vya ushirika, Dk. Benson Ndiege, kutengua maamuzi ya kufuta umoja wa vyama vya msingi (G 32 KNCI JV) vya wakulima na kurejesha kuendelea kufanyabishara ya kahawa kabla ya hatua za kinidhamu hazijachukuliwa dhidi yake.

Prof. Mkenda ametoa agizo hilo kufuatia hatua ya Mrajisi huyo kuufuta umoja huo kwa madai ya kwamba biashara ya kahawa inapaswa kufanywa na chama cha ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU) jambo ambalo sio sahihi.

Akizungumza leo Ijumaa Juni 18, 2021 wakati wa kufungua mkutano Mkuu wa 11 wa wadau wa kahawa nchini, uliofanyika jijini Dodoma, ambao uliandaliwa na bodi ya kahawa nchini (TCB), Waziri Mkenda, amesema umoja huo unapaswa kurejeshwa haraka na kuendelea na biashara ya kahawa kama ilivyokuwa hapo awali.

“Nimempa wiki moja Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini kuhakikisha G 32 wanarudi kufanyakazi ya biashara ya kahawa au yeye akose kazi….hawa wameungana na wanafanyabishara zao, KNCU sitaki ife Ila wakijiweka sawa wataendelea na wao,” amesema Prof. Mkenda.

Amesema KNCU inavyama vya msingi vya wakulima wa kahawa 95 na kwamba hawawasaidii wakulima, lakini jambo la kushanga G 32 imekuwa ukienda minadani na kufanya biashara pasipo kuwazuia.

“Mrajisi aliifuta G32 nikamuuliza kwanini na wakati KNCU bado haijakaa sawa ..KNCU inavyama 95 na haviwasaidii wakulima, Ila hawa G 32 wanafanyabiashara na wanasaidia wakulima vizuri na haiwazuii KNCU kuendelea na biashara…ninachotaka, sitaki KNCU ife warekebishe mambo yao alafu wote waungane ila kwa sasa bado,” amesema Prof. Mkenda.

Mbali na hilo waziri Mkenda amewaonya viongozi wa vyama vya ushirika kuacha ubadhirifu na kuwa na demokrasi ya kweli na kwamba kwa sasa serikali haitasita kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria.

“Kumekuwa na ubabaishaji mkubwa katika vyama vya ushirika na mimi nitaangalia na kusimamia sheria na viongozi mtawajibika….. sipendi kuweka watu ndani ila itabidi mlale korokoroni wakati mwingine,” amesisitiza Waziri huyo na kuongeza kuwa:

“Mwenge wa ushirika ulibebwa na KNCU na ukamulika nje ya mipaka yetu lakini wakauzima, lakini kama wameushika mwenge na wanatuonyesha njia kwamba inawezekana ushirika ukawepo maana wakulima bila ushirika haiwezekani,” amesema.

Awali, akizungumza katika Mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya kahawa, (TCB), Primus Kimaryo, alisema mkutano huo umekuwa ukifanyika kila mwaka kwa lengo la kukutanisha wadau na kuja na mikakati mbalimbali ya kukuza sekta ya kilimo cha kahawa chenye tija katika soko la dunia.

Naye mdau wa kahawa, Amir Amza, alisema wamekuwa wakikabiliwa changamoto mbalimbali ikiwemo tozo mbalimba ambaozo zimekuwa ni kandamizi ambapo aliiomba serikali kuondoa tozo hizo kwa lengo la kuendelea kuinua sekta ya kahawa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles