25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mbarawa achimba visima vitatu vya maji Kiteto

Mohamed Hamad

Waziri wa maji na umwagiliaji, Prof Makame Mbarawa ametimiza ahadi yake ya kuchimba visima vitatu vya maji mjini Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Ahadi hiyo ilitokana na Mbunge wa Jimbo la Kuteto, Emmanuel Papian CCM kumweleza Waziri Mbarawa kero ya maji inayowakabili wananchi wilayani humo.

Papian alisema wananchi wa mji wa Kibaya, ambako ni makao makuu ya Wilaya ya Kiteto wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji na kusababisha kutofanya shughuli zingine za maendeleo

“Mhe Waziri hawa wananchi wa Kiteto, Serikali tumefanikiwa kutoa huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 40% tu kiasi kilichobaki wanajitafutia wenyewe ambapo wanakunywa maji ambayo si safi na salama na kupata magonjwa mbalimbali tunaomba utusaidie kuchimba visima kupunguza adha hii,” alisema.

Prof Mbarawa akikagua mradi wa maji chini ufadhili wa The Islamic Foundation shule ya sekondari Kiteto, na mradi wa maji Kijiji cha Nchinila na Kazingumu baada ya kujionea hali ilivyo alitoa ahadi ya kuchimba visima vitatu vya maji.

“Nitahakikisha tunaondoa kero hii kwa kuchimba visima vya maji vitatu hapa kwani tatizo hili ni kubwa na linaweza kuleta madhara kwa wananchi,” alisema Mbarawa.

Visima vitatu vya maji vimechimbwa mjini Kibaya ambapo kimoja kipo eneo la mnadani, Kageze iliyopo Kijiji cha Bwagamoyo na Kaloleni mtaa wa Majengo mapya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles