25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

PROF. MAGHEMBE APINGA UKATAJI MTI MISITU YA AMANI

NA OSCAR ASSENGA-TANGA


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amepiga marufuku watu kuingia kwenye hifadhi ya misitu ya Amani iliyopo wilayani Muheza mkoani Tanga na kukata miti na wale watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Hatua hiyo imekuja baada ya uwepo wa taarifa za baadhi ya wananchi wilayani humo kuingia kwenye hifadhi hizo nyakati za usiku wakiwa na mashine ya kukatia mbao na kuamua kukata miti kinyume cha sheria.

Agizo hilo alilitoa juzi mjini Tanga wakati akifunga maonyesho ya tano ya Kimataifa ya Biashara yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwahako, ambapo alisema Serikali haipo tayari kuona msitu huo unaharibiwa.

Prof. Maghembe alisema misitu ya Amani ni muhimu kwa uhifadhi wa Taifa  kwani una bioanuwai  ambayo haipatikani mahali popote duniani  zaidi ya wilayani Muheza.

 “Hatutakubali kuona watu wanaingia kwenye hifadhi ya Misitu ya Amani na kukata miti  tutaweka askari kulinda na wale ambao wataingia usiku kwa ajili ya kwenda kukata miti huko watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola,” alisema Prof. Maghembe.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka wakazi wa Mkoa wa Tanga kujiandaa na fursa mbalimbali ikiwemo uwepo wa soda aishi  itakayotoka Ziwa Natroni na kuuzwa nchi za nje kupitia mkoani humo.

 “Hii ni fursa nzuri na muhimu sana kwa Mkoa wa Tanga hivyo wananchi wajipange kuona namna ya kuweza kuipokea na kuichangamkia,” alisema.

Waziri huyo pia alishauri Jiji la Tanga kuzungumza na Mali za Kale ili kuboresha maeneo ya Amboni ambapo kuna eneo yanatoka maji moto.

Awali akizungumza katika maonyesho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella, alimshukuru Waziri Maghembe kwa kufunga maonyesho hayo  muhimu kutangaza utalii na fursa zilizopo mkoani hapa.

Alisema kuna changamoto ya watu wanaoingia kwenye hifadhi ya misitu ya Amani kwa njia zisizo halali kuvuna misitu, wameichukua na wataweza kuifanyia kazi kwa mapana makubwa ili iweze kupata mafanikio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles