33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

PROF. MAGHEMBE AONYA UCHAGUZI WA CCM

Na MWANDISHI WETU-MWANGA


MBUNGE wa Mwanga mkoani Kilimanjaro, Profesa Jumanne Maghembe (CCM), amewataka wabunge kuepuka kupanga safu za uongozi ili kuepuka kukidhohofisha chama.

Profesa Maghembe ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema hayo hivi karibuni akiwa katika ziara jimboni kwake kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

“Kwenye jimbo langu uchaguzi unakwenda vizuri, huwa nahamasisha uhai wa chama kwa ujumla ndio mana utaona nilichangia fedha za kuimarisha majengo ya tawi. Nikiwa mbunge naepuka kujenga safu yaani kutafuta watu wangu na hili ninawahamasisha na wenzangu pia.

“Nahamasisha watu wote wawe na fursa za kuchagua na kuchaguliwa, watakaopatikana ndio tunaunda safu kuimarisha chama. Kwa sababu hiyo ndiyo maana katika Mkoa wa Kilimanjaro hapa Mwanga chama kipo imara kwa sababu mbunge wala viongozi wengine wa juu hawana makundi,” alisema Prof. Maghembe.

Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye ziara hiyo ya jimbo, Profesa Maghembe alisema kimsingi wamejiwekea malengo ya kutekeleza ilani ya chama kwa miaka mitano na kuainisha vipaumbele vya kuanza navyo.

Akieleza umuhimu wa elimu, Waziri huyo ambaye aliwahi kupewa dhamana ya kusimamia wizara ya elimu katika Serikali ya awamu iliyopita, alisema:

“Katika jimbo hili tumepiga hatua na sasa tunapeleka watoto 4,200 kujiunga na  sekondari kutoka watoto 300 hapo awali, pia tuna uhakika wa kuwa katika shule kumi bora zenye ufaulu mzuri kitaifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles