26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

PROF. KAMUZOLA AZUNGUMZIA HALI YA HEWA KWENYE UCHUMI

 

 

 

 

 

Na MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM


KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora, amesema mfumo wa kitaifa wa huduma za hali ya hewa (NFCS) mbali ya kutoa taarifa kwa wananchi kwa wakati pia utachochea ujenzi wa uchumi na viwanda nchini.

Prof. Kamuzora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usimamzi wa Maafa (TADMAC), aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini hapa, ambapo alipongeza hatua ambayo Tanzania imefika mpaka kuzindua mfumo huo kwani una nafasi kubwa katika kusaidia ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda kama azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojielekeza na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Profesa Petteri Taalas.

“NFCS ni mhimili mkubwa katika uchumi wa Taifa lolote duniani ikiwemo Tanzania, kwani unasaidia nchi au mtu kuwekeza kujiandaa kabla ya maafa kutokana na kupata taarifa kwa wakati.

“Jukumu letu kama Baraza ni kujiandaa na kuwa na maandalizi ya kutosha kutokana na maafa yoyote yatakayoweza kutokea nchini,” alisema Prof. Kamuzora.

Alisema mabadiliko ya tabia ya nchi ni makubwa duniani ambapo matokeo yake ni ukame, kuongezeka kwa kina cha bahari, uzalishaji mazao kupungua hivyo kupatikana kwa mfumo huu utasaidia kujiandaa na maafa yanayoweza kuepukika.

“Taarifa za hali ya hewa zitakazokuwa zinatolewa kupitia mfumo huu wa NFCS, zitasaidia kupunguza athari mbalimbali zitakazoweza kutokea,” alisema Prof. Kamuzora.

Alisema hii itasaidia kuongeza fursa ya ushiriki wa wananchi katika ujenzi wa uchumi kupitia kilimo na shughuli nyingine kwa kufuata taarifa za kitaalamu za hali ya hewa zitakazokuwa zikitolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), lengo ni kulinda nchi yetu na maafa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, alisema watekelezaji wa mfumo wa NFCS wapo katika Wizara yake hivyo ameahidi ushirikiano katika kutekeleza malengo ya mfumo katika kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinapatikana kwa usahihi na wakati.

“TMA inafanya vizuri katika utabiri wa hali ya hewa kwa asilimia 60 mpaka 70 ya taarifa wanazotoa zinakuwa sahihi, hivyo hii inaonyesha ni jinsi gani tumeboresha huduma zetu,” alisema Nditiye.

Alisema utendaji kazi wa Mamlaka ya hali ya hewa umeongezeka kwa kuwa na watu wenye weledi nakupelekea taarifa za hali ya hewa nchini kwenda vizuri na kwa kupitia mfumo uliozinduliwa hivi karibuni, tutaweza kuboresha zaidi huduma za taarifa ya hali ya hewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles