22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

Prof. Kabudi azindua mpango mkakati wa AZAKI na NGO’S

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Prof. Palamagamba Kabudi, amezindua Mpango mkakati wa Asasi za Kiraia (AZAKI) na Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) wa utekelezaji Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka mitano (2021-2026).

Uzinduzi huo umefanyika mapema leo Ijumaa Julai 2, 2021 jijini Dar es Salaam, siku tatu baada ya  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuzindua mpango wa tatu wa maendeleo, Juni 29, 2021 jijini Dodoma.

Mpango mkakati huo umeandaliwa na Mtandao wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), ikishirikiana na Azaki 300.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Prof. Kabudi amesema asasi hizo zina wajibu wa kukuza uchumi wa nchi kupitia miradi yake ya maendeleo, ili kuleta ustawi wa wananchi.

“THRDC  na mashirika yake zina nafasi kubwa katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi yetu katika huduma za kijamii, afya, elimu, maji na maeneo mengine muhimu ya haki za binadamu zinazohifadhiwa na Katiba ya 1977,” amesema Prof. Kabudi.

Aidha, Prof. Kabudi amezitaka asasi na NGO’s zisitegemee msaada wa fedha za wafadhili kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutekeleza miradi yake, huku akizishauri zibuni vyanzo vyake vya mapato. 

“Ili kuzifanya asasi za kiraia ziendelee, sio kila mwaka kuzipa fedha, bali kuziwezesha kupata fedha za kuanzisha vyanzo vya mapato. Ni wakazi wa asasi kutafuta njia nyingine kupata fedha kuliko daima kupendelea misaada. Sisemi tuache kutegemea misaada, bali tutafute vyanzo vyetu,” amesema Prof. Kabudi.

Mpango mkakati huo wa maendeleo wa Azaki na NGO’s unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021 hadi 2026.

Kupitia mpango huo, Azaki na NGO’s zinatarajia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa ya utoaji huduma za kijamii kwa wananchi, kupitia fedha za wafadhili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles