24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Kabudi ateta na mabalozi wateule wa Algeria

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, amekutana, kufanya mazungumzo na kupokea nakala za hati za utambulisho za balozi mteule wa Algeria hapa nchini, Ahmed Djellal pamoja na balozi mteule wa Ujerumani, Regine Hess.

Prof. Kabudi amekutana na mabalozi hao jana jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, kabla ya kukabidhiwa nakala za hati za utambulisho kukoka kwa mabalozi hao.

Katika mazungumzo hayo yaliyolenga kuimarisha uhusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria pamoja Shirikisho la Ujerumani.

Waziri Kabudi alimweleza Balozi mteule wa Algeria nchini kuwa Tanzania na Algeria zimeendelea kuwa na uhusiano mzuri na wa kihistoria tangu miaka ya 1960 wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika dhidiya ukoloni.

“Misingi ya uhusiano wa Tanzania na Algeria ulijengwa na Waasisi wa Mataifa haya mawili, Hayati Mwl. Julius Nyerere na Hayati Ahmed Ben Bella wa Algeria”Amesema Prof. Kabudi 

Alisema kuwa Algeria imeendelea kuwa na Ubalozi wake hapa nchini Tanzania tangu mwaka 1964 ikiwa ni miongoni mwa nchi zamwanzo kabisa kufungua ubalozi hapa nchini. Mwaka 1981 nchi hizi mbili zilianzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) ambayo imechangia kuimarisha na kukuza ushirikiano katika masuala mbalimbaliikiwemo diplomasia, ulinzi, elimu, madini, nishati na michezo.

Kwa upande wake Balozi mteule wa Algeria, Balozi Ahmed Djellal aliahidi kuwa Serikali ya Algeria itaendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania hususani diplomasia, kukuza na kuimarisha biashara, uwekezaji na utalii.

“Mimi Balozi Mteule nitashughulikia na kuhakikisha kwamba uwekezaji na biashara unaofanywa kati ya Algeria na Tanzania unakuwa wa manufaa kwa pande zote mbili lengo likiwa ni kukuza sekta ya biashara hapa Tanzania” alisema Balozi Djellal.

Katika tukio jingine, Prof. Kabudi amepokea nakala za hati ya utambulisho za Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani hapa nchini, Regine Hess ambaye amemweleza Waziri Kabudi kuwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Ujerumani ni mzuri na kuongeza kuwa jukumu lake kubwa kwa sasa ni kuendeleza uhusiano huo.

Balozi Regine  alisema kuwa mbali na uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani, ushirikiano mzuri uliopo wa uwekezaji, biashara, utalii na elimu utaendelea kuimarika na kutoa zaidi fursa zamaendeleo kwa Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles