23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Kabudi aeleza ushirikiano unaotakiwa Tanzania

LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema kwa sasa Tanzania inataka uhusiano wa kiuwekezaji zaidi kutoka nchi za nchi za Nordic badala ya kuendelea kupokea misaada.

Profesa Kabudi alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kikao na mabalozi mbalimbali kuhusu maandalizi ya mkutano wa 18 wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Afrika na Nordic unaotarajiwa kufanyika Novemba 7 na 8 hapa nchini.

Alisema mkutano huo unaotarajiwa kufunguliwa na Rais Dk. John Magufuli, tayari mawaziri 34 wa mambo ya nje wa nchi za Afrika wamealikwa kushiriki huku nchi zote tano za Nordic zikithibitisha kushiriki.

Nchi hizo za Nordic ni Sweden, Norway, Finland, Denmark na Iceland.

“Tangu walipokuja walijihusisha sana na elimu kwa wasichama, pia wavulana lakini pia na mambo ya afya,” alisema Profesa Kabudi.

Alisema ili kupata fedha si lazima kukusanya kodi tu bali pia kuchochea uchumi jambo litakalowezesha kupata mapato zaidi ya kodi na yasiyo ya kodi, yatakayowezesha kutoa elimu bila malipo, kujenga vituo vingi vya afya na mambo mengine.

 “Pia tutajadili uwezekaji na biashara kwa sababu sasa tunataka mahusiano yetu na Nordic yaache kuwa ya kupokea misaada tu, wametusaidia sana na tunawashukuru, lakini sasa tunataka kwende kwenye biashara na uwekezaji.

 “Na hii kwa Tanzania si mara ya kwanza hata wakati wa Awamu ya Kwanza Mwalimu alijaribu kuvutia uwekezaji kutoka nchi za Nordic, tulikuwa na kiwanda cha kuunganisha malori Kibaha,” alisema Profesa Kabudi.

Alisema kaulimbiu ya mkutano huo ni ushirikiano kwa maendeleo endelevu na unafanyika hapa nchini kutokana na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na nchi za Nordic ambao ulianza kabla ya uhuru wa Tanganyika baada ya kuja kwa wamisionari wa mataifa hayo baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles