Prodyuza atoa mchango kupitia kwa Ali Kiba

0
623

1NA MWANDISHI WETU

VIDEO ya ‘Lupela’ ambayo ni sehemu ya kampeni ya ‘Ujangili Unatuumiza Sote’ ya msanii Ali Kiba, imetengenezwa na mwandaaji filamu maarufu wa Hollywood, Brian Rumsey, ikiwa ni mchango wake kwa kampeni hiyo.

Video hiyo iliyochini ya WildAid na African Wildlife Foundation, imeongozwa na Kevin Donovan,

Mwandaaji huyo ameongoza video za wasanii wengi na maarufu nchini Marekani, akiwemo Rihanna na Sean Paul.

“Tuufanye mwaka 2016 mwaka wa tembo – mwaka ambao hatimaye tutakumbuka kuwa tulikomesha ujangili wa tembo na kuwapa tembo nafasi ya kuishi. Tusaidie kuokoa maisha ya wanyama hawa wazuri,” alisema Kiba.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here