24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

PRIYANKA CHOPRA, JONAS KIMEELEWEKA


NEW YORK, MAREKANI

HATIMAYE staa wa filamu na muziki nchini Marekani, Priyanka Chopra, amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Nick Jonas baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha miezi miwili.

Wawili hao wamekuwa wakionekana wakiwa pamoja kwenye matamasha mbalimbali na kuwafanya mashabiki wabaki na maswali, lakini majibu yake yamepatikana baada ya mrembo huyo kuthibitisha kuvishwa pete ya uchumba.

“Nina furaha kwa maamuzi ya Nick Jonas ya kuamua kunivisha pete ya uchumba, alifunga safari hadi jijini New York kwa ajili ya kwenda kuifuata na sasa kila kitu kipo wazi, sikuwa tayari kuweka wazi kwa mashabiki kabla ya mipango kukamilika, lakini sasa ninaweza kuongea, nampenda sana Nick,” aliandika mrembo huyo.

Priyanka mwenye umri wa miaka 36, raia wa nchini India, amedai yupo tayari kufunga ndoa na mpenzi wake huyo mwenye umri wa miaka 25 bila ya kujali tofauti ya umri wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles