30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Prisons yampiga mtu 6-1

Na WINFRIDA MTOI- DAR ES SALAAM

TIMU ya Tanzania Prisons, imetoa kichapo cha mabao 6-1 kwa Karasha ya Ligi Daraja la Tatu, katika mchezo wa kirafiki uliopigwa juzi kwenye dimba la Sokoine, Mbeya.

Mchezo huo ni maandalizi ya kuelekea katika  mchezo wa mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo maafande hao wa Jeshi la Magereza wananatarajia kuumana na JKT Tanzania,  Juni 23 mwaka huu.

Kabla ya mchezo huo, Prisons ilijipima na Mbeya City pia ya Ligi Kuu na kulazimishwa suluhu.

Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Mkuu wa Prisons, Mohammed Rishard ‘Adolf’, alisema  ameridhishwa na maendelea ya kikosi chake na kuahidi kusaka timu nyingine za kujipima ubavu.

“Tumecheza mechi nyingine ya kirafiki na Karasha FC, tumeshinda 6-1, vijana wangu wanajitahidi, ila atujafikia malengo hasa katika safu ya ushambuliaji,” alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,873FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles