23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Primier Sekondari na mkakati wa kukomboa wanafunzi

Wanafunzi wakiwa kwenye majaribio kwa vitendo somo la kemia.
Wanafunzi wakiwa kwenye majaribio kwa vitendo somo la kemia.

Na Mwandishi Wetu,

KWA kipindi kirefu shule nyingi za sekondari zinapokea wanafunzi wengi ambao wamehitimu darasa la saba, wakiwa na uwezo mdogo wa kuzungumza lugha ya Kiingereza.

Hali hiyo, huwafanya walimu wengi hasa wa shule binafsi kuwa na kazi ya ziada ya kuwafundisha na hali hii inachangiwa mno  na wazazi wengi kutoshirikiana vyema na walimu katika kusimamia maendeleo ya watoto wao.

Kutokana na hali hiyo, MTANZANIA ilifanya mahojiano hivi karibuni na  Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Primier, Aysha  Mzee wa shule ya sekondari Premier Girls iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Anasema shule za sekondari zinapokea wahitimu walipata misingi mizuri ya elimu, lakini pia zinapokea ambao hawana misingi mizuri kwa ajili ya kumudu vyema masomo ya sekondari.

“Jambo hili ni changamoto kubwa,tunapokea baadhi ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba wakiwa na uwezo mdogo ambao kama tukiwaacha walivyo inakuwa ngumu kumudu masomo ya sekondari.

“Hali hii,inasababisha walimu wa shule za sekondari ikiwamo yangu kutumia muda mwingi kufundisha muda wa ziada mada zitakazowasaidia wamudu masomo, hasa mwaka wa kwanza,”anasema Aysha.

Anasema hali hiyo, ndiyo inafanya baadhi ya shule za bianfsi kupendelea kuchukua wanafunzi ambao wamefanya vizuri katika masomo yao ya kuhitimu darasa la saba tu.

“Sisi katika shule yetu, tunaona jambo hili ni kama ubaguzi,ndiyo maana tunalazimika kuwapa nafasi wanafunzi wote na kuhakikisha tunawapika vya kutosha ili kumudu masomo ya sekondari,”anasema Aysha.

Anasema jambo hilo, limewasukuma kuweka mikakati ya kuimarisha utoaji wa elimu bora zaidi kwa kuhakikisha wanawajengea uwezo wanafunzi ili wawe na utayari wa kujifunza.

“Wanafunzi wengi wanapata taabu kwenye lugha ya kufundishia ambayo ni Kiingereza.

“Nikiri  lugha ya Kiingereza bado ni tatizo kubwa kwa wanafunzi wetu wanaohitimu darasa la saba. Serikali ya awamu ya tano inalo jukumu la kusaidia kuboresha eneo hili katika shule za msingi ili wanafunzi wanapojiunga na elimu ya sekondari wawe na uwezo wa kutambua kile wanachojifunza kupitia lugha inayotumika,” anasema Aysha.

Anasema kutokana na hali hiyo,shule walimu wa shule yake,hulazimika kuwa na mpango maalumu wa kufundisha lugha hiyo baada ya masomo ya darasani.

“Unajua Premier Girls ni shule ya bweni,tumejitahidi kuweka miundombinu yote muhimu ya kujifunzia na kufundishia.

“Tumejipanga vizuri, shule ina maktaba ya sayansi, maabara ya kompyuta,madarasa ya kisasa pamoja na mtandao wa maji ya uhakika na umeme,vitu ambavyo vinatupa uhakika wa kutoa elimu bora.

“Tunajitahidi kuwa na walimu mahiri waliotoka vyuo vikuu kwani tunaamini wana uwezo mkubwa zaidi wa kufundisha na kutuletea mafanikio kwa matokeo ya kidato cha nne na cha sita kama yalivyo sasa. Kwa hii changamoto inabakiwa kwa wanafunzi ambao kama nilivyosema baadhi yao msingi wao walioupata wakiwa elimu ya msingi sio mzuri,”anasema Aysha.

Anasema pamoja na kuwajengea uwezo walimu wao na kuwafanya watekeleze majukumu yao kwa ufanisi, wamekua pia wakishiriki katika mafunzo mbalimbali na kufanyiwa tathmini ya mara kwa mara.

“Tunafanya tathmini ya namna walimu wanavyofundisha na namna wanafunzi wanavyopokea maarifa na stadi mbalimbali. Haya yamefanyika na kutuletea  matunda mazuri yanaonekana.

“Mwaka 2011 tulipokea wanafunzi 18 wote walikwenda vyuo vikuu anasema,mwaka 2013 matokeo yetu tulikuwa shule ya tisa  kati ya 379 Kanda ya Mashariki, tulipata wastani wa 83 na kuingia 10 bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles