26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Prezzo: Nimechoka kusimangwa

PrezzoNAIROBI, KENYA

MKALI wa muziki nchini Kenya, CMB Prezzo, amesema kutokana na kuandamwa sana katika mitandao ya kijamii kutokana na aliyoyatenda katika matukio mbalimbali kwa sasa ameamua kuachana nayo na kuja kivingine ili kuwashawishi upya mashabiki wake.

Msanii huyo amesema amekuwa kimya kwenye mitandao ya kijamii na kazi zake za muziki kutokana na tukio ambalo alilifanya kwa mtangazaji wa runinga ambapo alionesha utovu wa nidhamu mwanzoni mwa mwaka huu, lakini amedai kubadilika.

“Najua niliwakosea wengi mapema mwaka huu, lakini mimi ni binadamu na sijakamilika, nadhani huu ni wakati wangu wa kuwarudisha mashabiki katika muziki wangu.

“Ninachotaka kukifanya kwa sasa ni kuachia nyimbo kali ili kuwafanya mashabiki wangu kuwa pamoja, kuna kazi inakuja ambayo nimefanya na Bamboo, ninaamini itapokelewa vizuri,” alisema Prezzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles