PREZZO AWACHIMBA MKWARA WANAUME KENYA

0
522

NAIROBI, KENYA


MKALI wa muziki nchini Kenya, Jackson Makini ‘CMB Prezzo’, amewachimba mkwara wanaume wa nchini humo wanaomfuatilia mpenzi wake wa zamani, Michelle Yola.

Msanii huyo amedai kuwa, japokuwa ameachana na mpenzi huyo, lakini bado wapo kwenye mazungumzo ya kutaka kuyaweka mambo sawa ili warudiane, hivyo mwanamume yeyote anayejaribu kumshawishi mrembo huyo waweze kuwa kwenye uhusiano atahakikisha anapambana naye.

“Ni kweli nipo kwenye mgogoro na Michelle katika uhusiano wetu, bado sijatangaza kama tumeachana, japokuwa kuna habari kwenye mitandao zinadai tumeachana.

“Mazungumzo yanaendelea kwa ajili ya kuweka sawa mgogoro wetu, hivyo sipo tayari kuona mwanamume mwingine akijipeleka kutaka kuanzisha uhusiano na Michelle,” alisema CMB Prezzo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here