25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

PPRA yatangaza kiama kwa maofisa masuhuli

Dk. Martin Lumbanga
Dk. Martin Lumbanga

Na Gabriel Mushi, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), imesema itawachukulia hatua za  sheria baadhi ya maofisa masuhuli wa taasisi za umma kwa kufanya ununuzi wa Sh bilioni 8.5 kwa mwaka wa fedha 2014/15 kinyume cha Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011.

Pia maofisa hao wameshindwa kuwasilisha mipango ya Ununuzi ya mwaka 2015/16 (GPN) kwa ajili ya kuchapishwa kwenye jarida la ununuzi wa umma pamoja na tovuti ya PPRA.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Dk. Martin Lumbanga, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu taasisi za umma 361 zilizokaidi kutekeleza matakwa ya sheria ya ununuzi.

Alisema tangu mwaka wa fedha 2016/17 uanze Julai, mosi mwaka huu, ni taasisi za umma 145 (asilimia 28.6) kati ya taasisi 506 zilizopo ambazo zimekwisha kuwasilisha mipango yao ya ununuzi kwa mujibu wa sheria.

Alisema kanuni ya 70 ya ununuzi wa umma ya mwaka 2013 inaitaka taasisi wanunuzi kuandaa na kuwasilisha kwa PPRA mpango wa ununuzi wa mwaka ndani ya siku 14 baada ya kumalizika kwa mchakato wa bajeti.

Alisema sheria hiyo inaelekeza mipango yote ya ununuzi kuchapishwa kwenye jarida hilo la PPRA ndani ya mwezi mmoja kabla ya kuanza mchakato wa zabuni zilizopo kwenye mipango ya ununuzi kwa mwaka wa fedha husika.

“Lengo la matakwa ya  sheria ni pamoja na kuongeza uwazi na ushindani katika ununuzi ua umma, kutoa fursa kwa wazabuni kushiriki zabuni kwa haki na usawa   kupata thamani bora ya fedha kwenye ununuzi wa umma na   kuiwezesha PPRA kutekeleza jukumu lake la udhibiti na usimamizi.

“Taasisi zilizowasilisha ni chache, tatizo hili limechangia kuwapo  upotevu wa fedha za umma kutokana na taasisi nunuzi kuingia mikataba ya ununuzi isiyo na tija, kuwapo   vitendo vya rushwa, ukiukwaji wa sheria ya ununuzi na ufifishaji wa jukumu la PPRA la usimamizi na udhibiti,” alisema.

Alisema miradi mingi yenye thamani kubwa iliyofanyiwa uchunguzi na PPRA na kubainika kuwa na upungufu mkubwa  haikuwa imejumuishwa kwenye mpango wa ununuzi wa mwaka wa taasisi husika.

“Ndiyo maana taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2014/15, ilibainisha  ununuzi wa Sh bilioni 8.5 haukuwa umejumuishwa kwenye mpango wa ununuzi, tunafanyia kazi na kuwachukulia hatua maofisa masuhuli wote wa taasisi za umma waliokiuka sheria,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa PPRA, Dk. Laurent Shirima alisema taasisi nyingi za umma zimekuwa zikikwepa kuchapisha mipango ya ununuzi kwenye jarida la PPRA na kupeleka katika magazeti mengine kitendo kinachoonyesha  kuwapo  vitendo vya rushwa na malalamiko kwa wananchi.

“Dhana ya maelekezo haya ya sheria ni kuwa na kitovu kimoja cha wazabuni wanaotarajiwa kushiriki zabuni za umma kupata taarifa za zabuni zitakazopitishwa na serikali na taasisi zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles