25.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Posta waja na stempu kutangaza vivutio vya utalii

Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na Shirika la Posta la Oman wamechapisha stempu maalumu yenye vivutio mbalimbali vya utalii.

Stempu hiyo itazinduliwa Oktoba 9,2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani.

Akizungumzia maadhimisho hayo Msemaji wa Shirika la Posta, Elia Madulesi, amesema wanaunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya utalii ndiyo maana kwa wamechapisha stempu hiyo.

“Stempu hii itakwenda katika nchi 192 ambazo Shirika la Posta Tanzania ni mwanachama, itakuwa na vivutio vya wanyama hivyo tutatangaza utalii wetu,” amesema Madulesi.

Amesema pia kutakuwa na kongamano kujadili biashara mtandao na anwani za makazi sambamba na kujadiliana wapi walikotoka, walipo na wanapokwenda.

Naye Meneja Barua na Usafirishaji wa shirika hilo, Jason Kalile, amesema shirika hilo kwa sasa limejikita katika mageuzi ya kiteknolojia na kwamba wakati wa maadhimisho hayo pia watazindua huduma mbalimbali za kidigitali ikiwamo ya posta kiganjani ambayo inamwezesha mteja kupata huduma kirahisi kupitia simu janja.

Mwaka jana shirika hilo lilizindua duka mtandao linalomwezesha mteja kuagiza vitu kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Katika maadhimisho hayo pia washindi wa mashindano mbalimbali yaliyoandaliwa na shirika hilo watazawadiwa.

Mashindano hayo pamoja na uandishi wa barua kwa wanafunzi chini ya miaka 18, uandishi wa insha, uandishi wa makala kwa wanahabari, ubunifu wa mifumo ya tehama katika mawasiliano ya post ana ubunifu wa video inayotumia vibonzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,718FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles