29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Posta Arusha kutoa msaada Gereza la Kisongo

Na Mwandishi Wetu, Arusha

SHIRIKA la Posta Mkoa wa Arusha limepanga kutembelea na kutoa misaada kwa watoto wenye uhitaji katika Gereza Kuu la Kisongo,mkoani hapa.

Licha ya kutembelea watoto hao,Shirika hilo litatumia nafasi hiyo kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali inazotoa kwa wananchi.


Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake,Meneja wa Shirika hilo mkoani hapa, Athman Msilikale,amesema wanatarajia kutoa misaada hiyo Oktoba 9, mwaka huu wakati wa maadhimisho ya siku ya Posta duniani.

Amesema maadhimisho haya ambayo kitaifa yatafanyika jijini Dodoma,yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu kwa Posta Endelevu”.

Amesema kutokana na shirika hilo kuwa la serikali hivyo linashirikiana na wananchi na kuwa mkoani hapa wameona kwa kuwa wanapaswa kurejesha faida kwa jamii,kutumia maadhimisho hayo kukutana na kundi hilo la watoto ambao wanaishi katika mazingira hayo.

“Lengo ni kuwafariji ili wasijione wametengwa na jamii,hasa baada ya wengine wazazi wao kuhukumiwa,tunapaswa kutambua kuwa wana mahitaji hivyo tunatatoa misaada kulingana na mahitaji yao,”amesema meneja huyo.

“Hili ni shirika la serikali,tunaona ni muhimu tuipeleke kwa wananchi kwa sababu tunaona ni vizuri tukashirikiana na wananchi kwa pamoja,”amesema.

Kuhusu elimu kwa jamii amesema watatumia fursa hiyo kuelezea huduma zao za posta ambazo wamekuwa wakizifanya ikiwemo utumaji wa barua,nyaraka na vifurushi kupitia huduma ya EMS.

Ameeleza kuwa shirika hilo la Kimatiafa lina mtandao mkubwa kuanzia kidunia, Afrika tuna kuliko mashirika mengine ambapo duniani kuna vituo vya kutoa huduma zaidi ya 600,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles