Pope: Mo atatufanya tupumue

POPE1Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI  wa Kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope, amesema kwamba kwa sasa klabu hiyo na Kamati yake itapumua katika kupangilia fedha za maendeleo na  usajili wa wachezaji unaoendelea ili kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Kauli hiyo inakuja baada ya mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji ‘Mo’ kutoa kitita cha Sh milioni 100 katika klabu hiyo ili kusaidia usajili wa wachezaji ikiwamo kupata saini ya mshambuliaji, Muivory Coast, Fredrick Blagnon.

Uamuzi huo wa Mo ulifanyika huku akisubiri mchakato wa kupewa umiliki wa asilimia 51 za hisa ukamilike ili aweke Sh bilioni 20, ikiwa ni moja ya malengo ya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo kutoka hatua ya kutumia kadi  hadi hisa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Pope alisema ingawa walikuwa wakifanya usajili, walikuwa wakijibana katika maeneo mengine ili kufanikisha usajili na shughuli nyingine za maendeleo ya klabu hiyo.

“Tulipoanza usajili hatukuwa na fedha za Mo ila kwa fedha zetu, ikizingatiwa kwamba tulikuwa tukijibana sehemu nyingine ili kufanikisha zoezi hilo lakini kwa sasa baada ya ujio wake tutapumua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here