25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

POMBE ZA VIROBA ZAITWA ‘NGURUKA’

Na RAMADHAN LIBENANGA- MOROGORO

WAFANYABIASHARA wa vileo mkoani Morogoro, wamebadili jina la pombe inayofungashwa katika mifuko ya plastiki maarufu viroba kwa kuiita ‘nguruka’ kukwepa mkono wa sheria.

Nguruka ni jina ambalo linatumika kwa wenyeji kuogopa kutaja jina la kiroba na linajulikana kwa wengi katika Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake.

Katika baadhi ya mitaa, MTANZANIA limebaini kwa sasa watumiaji wa pombe hizo wamebuni jina hilo waweze kuendelea na biashara hiyo bila kujulikana na vyombo vya dola na mamlaka nyingine zinazohusika na ukamataji huo.

Mmoja wa watumiaji wa kinywaji  hicho  aliyejitambulisha kwa jina la Majaliwa Masepu, mkazi wa Msamvu, alisema:   

 “Sasa hivi ukienda baa au dukani unatakiwa kusema naomba ‘nguruka’, muuzaji atakuuliza unataka  nguruka wakubwa au wadogo, maana kuna aina mbili za ujazo wa viroba.”

Masepu alisema hatua ya Serikali kuzuia pombe hiyo imeathiri wafanyabiashara na watumiaji kwa kuwa imekuwa ghafla mno kiasi cha kutishia wafanyabiashara wengi kufilisika ikizingatiwa walikuwa na mzigo mkubwa katika maghala yao.

“Ni vema Serikali ingetupatia muda hata wa miezi  mitatu kumaliza mzigo wetu,” alisema mfanyabiashara mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei, alisema msako huo wa viroba unaendelea na watachukuliwa hatua wafanyabiashara wanaokaidi agizo hilo kwa kuendelea kuuza viroba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles