POMBE YAUA 26 MKESHA WA KRISMASI PAKISTAN

0
744

ISLAMABAD, PAKISTAN


pombe-pakistanPOLISI nchini Pakistan wamesema watu 26 wamefariki dunia baada ya kunywa pombe haramu usiku wa kuamkia Krismasi.

Ofisa wa polisi katika mji wa Toba Tek, Muhammad Nadeem, amesema kuwa kundi la watu katika mji huo uliopo kilomita zaidi ya 330 kusini mwa Islamabad, walitengeneza kileo haramu na kunywa wakati wa mkesha huo.

Alisema kuwa watu 19 miongoni mwa waliokufa walikuwa ni Wakristo na wawili walikuwa Waislamu.

Baadhi ya ripoti zinasema kuwa wengine zaidi ya 100 waliokunywa pombe hiyo wanapata matibabu hospitalini.

Kutokana na uuzaji wa pombe kudhibitiwa nchini Pakistan, pombe za bei ya chini zenye sumu zimekuwa zikitengenezwa majumbani mwa watu.

Oktoba mwaka huu watu wengine 11 walifariki dunia katika Jimbo la Punjab baada ya kunywa pombe yenye sumu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here