24.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Polisi yawachukulia hatua Komedi kwa kuvaa sare zao

vengu original comedy

NA MWANDISHI WETU

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema linachukua hatua za kisheria dhidi ya wasanii wa kundi la kisanii la ‘Original Comedy’ kutokana na kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Advera John Bulimba, Jeshi hilo limetoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia  mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na  majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yake.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza zaidi kwamba kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, sura ya 16 na  marejeo yake ya mwaka 2002,  kifungu cha 178 (1) na (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama,  kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye si mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo  bila kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivi karibuni wasanii wa kundi hilo walivaa mavazi hayo wakati walipokuwa katika sherehe ya harusi ya msanii mwenzao wakati ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu za nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles