24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi yavamia ofisi za CUF, yakamata viongozi tisa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani Mtwara kuvamia ofisi za chama hicho na kuwakamata wanachama tisa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Naibu Mkurugenzi Habari na Uenezi wa CUF, Abdual Kambaya, ilisema Machi 12, mwaka huu kati ya saa saba mchana hadi saa 10 jioni, polisi walifika katika ofisi za chama hicho na kupekua bila kusema wanatafuta nini.
“Walipekua ofisi na baadaye walihamia katika nyumba za wanachama mbalimbali na kuendeleza upekuzi wao, leo hii (jana) wameendelea na kamatakamata yao na kumkamata Mwenyekiti wa CUF Wilaya, Salimu Mchumbila na Katibu wake, Saidi Kulagha ,” alisema Kambaya.
Alisema wanachama hao walichukuliwa na polisi na kupelekwa kusikojulikana.
“CUF Taifa tulipopata taarifa hiyo tulianza kufuatilia na RPC wa Mtwara alisema hana taarifa ya tukio hilo,” alisema Kambaya.

Alisema CUF kina taarifa za ndani kuwa baadhi ya wanasiasa mkoani humo wanahusika na ukamataji huo ili kudhoofisha chama hicho katika kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.
“CUF kama chama tunasema mchezo huu hautafanikiwa na tunawahidi na kuwahakikishia kuwa hawataweza, tunalaani kitendo hiki cha polisi kuendelea kutumiwa na CCM kuisaidia harakati zake,” alisema Kambaya.
Alisema kwa sasa chama hicho kinaendelea kufuatilia walipo vijana hao na baadaye watatoa tamko la hatua gani watachukua dhidi ya jambo hilo.
Aliwataja wanachama wengine waliokamatwa kuwa ni Mjumbe Mkutano Mkuu, Ismail Njalu, Mwenyekiti wa Vijana, Sadick Songoni, Katibu Kata Vijae, Ahmed Kisewe.
Wengine ni Mwenyekiti Uhamasishaji/Mjumbe wa Kamati Tendaji, Seleman Nandondende, Mjumbe wa Kamati Tendaji, Iron Lankila, Mkurugenzi wa BG, Yasin Okororo na Mjumbe Said Mtondo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles