27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

POLISI YATHIBITISHA NABII TITO MGONJWA WA AKILI

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limesema Tito Machibya (44), maarufu Nabii Tito ambaye anashikiliwa na jeshi hilo kuwa ni mgonjwa wa akili.

Nabii huyo ambaye amejipatia umaarufu hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, baada ya kusambaa kwa video inayomuonesha Nabii huyo akicheza muziki akiwa pamoja na wanawake wawili ambao anadai kuwa ni mke wake pamoja na mfanyakazi wake wa ndani ambapo pia anahamasisha watu kuwa na uhusiano wa aina hiyo sanjari na kunywa pombe kwani si dhambi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amewaambia waandishi wa habari kuwa  baada ya uchunguzi uliofanywa na Dk. Dickson Philipo wa Hospitali ya Milembe mkoani hapa wamegundua kwamba mtuhumiwa huyo ni mgonjwa wa akili kwa muda mrefu.

Kamanda Muroto amesema Nabii Titoo aliwahi kufanyiwa uchunguzi Juni 6, mwaka 2014 katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili na kugundulika ana ugonjwa wa akili.

“Katika hospitali hiyo alitibiwa magonjwa ya akili ambapo aliruhusiwa kutoka wodini na daktari wake Dk.William ambapo alitakiwa kurejea tena kwa uangalizi wa tiba Julai 9, mwaka huo huo lakini hakurejea.

“Baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa anaonekana Dodoma akifanya vitendo vya kidhalilishaji na kupotosha jamii ndipo tulimkamata na kumpeleka katika Hospitali ya Milembe kwa uchunguzi zaidi tumegundua kwamba ni mgonjwa wa akili kwa muda mrefu,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, Kamanda Muroto ameshangazwa kwamba pamoja na kuwa na hali hiyo lakini ameendelea kuhamasisha maovu ambayo ni kinyume na desturi za Watanzania huku akionekana ni mtu mwenye akili timamu huku watu wakimshabikia.

Amesema Jeshi la Polisi litawachukulia hatua kali watu wa aina hiyo au wanaombatana nao kwani ni kinyume na tamaduni za Kitanzania.

Kamanda Muroto alisema wanaendelea kumshikilia Nabii huyo kwa ajili ya upepelezi zaidi ili kunusuru maisha yake.

Akiwa kituoni hapo Nabii Tito amesema mambo yote anayoyazungumza na kuyafanya anayotoa katika Biblia na katika kanisa lake waumini wake lazima wawe na shepu na sura nzuri kwa sababu anahitaji kuwa na watu wa aina hiyo ambao nao watasadiki kile anachokizungumza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles