29.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Polisi yaomba wazazi kukagua watoto wao sehemu za siri

FRANCIS GODWIN -IRINGA

KUTOKANA na Jeshi la Polisi mkoani Iringa kumshikilia mwalimu wa masomo ya ziada,  Anord Mlay kwa tuhuma  za kulawiti watoto zaidi ya 24, jeshi hilo limewataka wazazi na walezi kuanza  kuwakagua sehemu zao za siri watoto pasipo  kuwaonea aibu ili kujua kama wamefanyiwa  vitendo vibaya.

Limesema watoto wengi wamekuwa wakifanyiwa ulawiti na ubakaji hukaa kimya bila kutoa taarifa kwa wazazi wao.

Akizungumza wakati wa mdahalo wa amani, uzalendo na ushirikishwaji wa vijana, wanawake na watu  wenye ulemavu katika masuala mbalimbali ya  maendeleo jana, ulioandaliwa na Mwamvuli wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Iringa (ICISO) kwa  kushirikiana na Ushirika  Tanzania, Ofisa wa Polisi Ushirikishwaji Jamii, Vicent Msami alisema tukio la mwalimu   kulawiti watoto zaidi ya 24, ni la kutisha na linawapa somo wazazi kuanza ukaguzi wa  watoto wao.

Msami alisema mtuhumiwa anaonyesha alianza kufanya vitendo hivyo kati ya mwaka 2015 na 2019.

Alisema idadi hii ni kubwa na kuna uwezekano ikaongezeka endapo wazazi watajitokeza.

“Mtuhumiwa alikuwa anatumia mbinu ya kuwawekea watoto picha  za ngono zinazofundisha  namna ya watu kufanya mapenzi, baada ya  watoto kuangalia anawalazimisha kufanya nao mapenzi mmoja baada ya  mwingine,” alisema Msami.

Alisema kumchunguza  mtoto kama yupo vizuri  kiafya ni jukumu muhimu na kuendelea  kumwonea aibu ni mwanzo wa kumwathiri  mtoto.

Alitaka jamii kujenga  utamaduni wa kuongea na watoto wao mara kwa mara ili kujua kama  wameanza kuchezewa  na watu wabaya.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ameunda kamati ya watu 10 kufuatilia na kubaini watoto ambao wamefanyiwa ukatili.

Baadhi ya wazazi wa  watoto, wanadai mwalimu huyo pia alikuwa anatumia mbinu ya kuchezesha michezo ya watoto kupitia  kompyuta (game)  kuwarubuni wengi zaidi kufika eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles