24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi yachunguza vijana kujiunga Al-Shabaab, IS

Mkurugenzi wa Upelelezi wa  Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman

Patricia Kimelemeta na Asifiwe George, Dar es Salaam    

JESHI la Polisi nchini, limesema linafanya uchunguzi kubaini baadhi ya vijana wanaojiunga na vikundi vya kigaidi, vikiwamo IS na Al-Shabaab ili wawachukulie hatua za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa  Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman, alisema wimbi la vijana hao kujiunga na makundi hayo yanayopigwa vita duniani kote, linatokana na ushawishi wa baadhi ya watu.

“Tuna taarifa za kuwapo baadhi ya vijana wa Kitanzania wanaojiunga na vikundi vya ugaidi… suala hili ni la kiintelijensia zaidi, hatuwezi kulizungumzia kiundani, tunaendelea kulifanyia kazi, tutakapofikia sehemu nzuri tutawaambia,” alisema Athuman.

Alisema wakati suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi, jeshi hilo liliendesha operesheni maalumu ya siku mbili, ambayo ilishirikisha nchi 26 za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Alizitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Lesotho, Malawi, Madagascar, Mauritius, Msumbuji, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia, Zimbabwe, Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Shelisheli, Sudan Kusini na Somalia.

Alisema operesheni hiyo iliyojulikana kama ‘Operesheni Usalama III’ ilishirikisha nchi zaidi ya 26 na ilisaidia kukaguliwa kwa magari 1,632 ambayo kati ya hayo, 10 yalikuwa ya wizi huku matano yalibainika yameingiliwa ‘chases’.

Alisema operesheni hiyo pia ilisaidia kukamatwa  pikipiki 12 za wizi, huku 18 zikiendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kutokuwa na vibali halali.

Athuman alisema operesheni hiyo ilisaidia pia kukamatwa aina mbalimbali ya dawa za kulevya, zikiwamo heroine gramu 83, bangi kilogramu 398.6, mirungi kilogramu 30, bunduki aina ya shotgun moja, gobole 11, risasi 104, mkuki mmoja na vipande 15 aina ya exprojel v6, cotex na detonator.

Alisema walikamata wahamiaji haramu 43  maeneo mbalimbali nchini, kati yao 18 ni raia wa DRC, ambao walikamatwa mikoa ya Rukwa na Kagera, wakati 22 wanatoka Burundi waliokamatwa mikoa ya Shinyanga, Tabora na Kagera na raia wawili wa Rwanda walikamatwa Kagera na mmoja wa Kenya alikamatwa Tabora.

“Katika operesheni hii tulifanya ukaguzi katika kampuni mbalimbali zinazofanya biashara ya madini ambapo tatu zilionekana kukosa uhalali wa kupewa leseni ya kuendelea kufanya biashara ya madini,

“Kampuni hizi ni Delicore Metal Company Ltd, Madandwa Gold Mining Export Import (T) Ltd na Alex Mining Co. Ltd, na tatizo lao linaendelea kushughulikiwa na Wizara ya Nishati na Madini. Pia yalikamatwa madini aina ya Acquqmiline Smoky Quartz kilogramu 20.

Alisema pia walikamata gamba moja la kasa mkoani Ruvuma, mbao 410 zilizokuwa zikisafirishwa bila kibali mikoa ya Pwani, Iringa na Morogoro, nyama ya pundamilia kilo 45 na bidhaa bandia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles