24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WAVURUGA MKUTANO WA WAANDISHI, CHAMISA

Harare, Zimbabwe


Polisi wamevunja mkutano wa waandishi wa habari na kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa uliokuwa ukifanyika huko Harare leo saa chache baada ya Rais Emmerson Mnangagwa kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais, ambapo kiongozi huyo  alikuwa akipinga matokeo ya uchaguzi.

Chamisa alizungumza muda mfupi baada ya polisi kuvunja mkutano wake na waandishi wa habari wa wakisubiri taarifa yake.

Chamisa, ambaye alipata asilimia 44 ya kura, anasema vurugu na unyanyasaji unafanyika dhidi ya wafuasi wake na udanganyifu wa matokeo ya uchaguzi.

Kiongozi huyo amesema upinzani wana ushahidi wa uharibifu wakati wa kupiga kura lakini tume ya uchaguzi hawataki kuwasikiliza.

“Tulishinda uchaguzi huu na tunamsihi Mnangagwa kukubali hilo,” amesema.

Mara baada ya tukio hilo Rais Mnangagwa haraka alikemea hatua hiyo ya polisi na kusema matukio ya polisi kupigana na waandishi wa habari ambao wanasubiri taarifa hayana nafasi katika jamii yetu.

Katika ukurasa wake wa Twitter Rais Mnangagwa aliandika mamlaka husika ichukue hatua na ichunguze haraka tukio hilo. Na kuongeza kwamba; “tulishinda uchaguzi kwa uhuru na haki, na hatuna chochote cha kujificha.”

 

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles