25.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Polisi waua majambazi wawili Dar

andrew sattaNa Asifiwe George, Dar es Salaam

WATU wawili wanaodhaniwa kuwa  ni majambazi wamefariki dunia  wakati wa majibizano ya risasi na polisi katika eneo la kiwanda cha SuperDoll,  Barabara ya Nyerere,  Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea   jana mchana wakati mtu mmoja ambaye hakufahamika jina akitokea katika Benki ya Amana eneo la Banda la Ngozi, akiwa na fedha,  alipovamiwa na watu wasiofahamika  wakiwa na pikipiki  na kutaka kumpora fedha hizo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,   katika harakati za kumpora mtu huyo, watu hao waliweza kuchukua fedha hizo na kukimbia nazo  huku baadhi ya waendesha bodaboda wakiwafukuza kwa nyuma.

Inaelezwa kuwa walipofika katika eneo la kiwanda cha SuperDoll,   polisi na majambazi  hayo walifyatuliana  risasi na   kuwaua majambazi wawili, huku mmoja akiwa na silaha na mfuko wa fedha walioupora akikimbilia katika kiwanda cha mabati kilichopo   Tabata.

Hata hivyo, mashuhuda hao walisema hadi kufikia saa nane mchana, polisi walikuwa wakiendelea kufanya msako katika kiwanda hicho ikidhaniwa kuwa  jambazi huyo  alikuwa amejificha humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Andrew Satta, alikiri kutokea   tukio hilo.

Hata hivyo, hakuweza kulizungumzia tukio kwa undani  akisema kuwa  vijana wake walikuwa bado wako eneo la tukio.

Alisema angelizungumzia suala hilo  baada ya kupata taarifa kutoka kwao  na akaomba apigiwe baada ya muda kidogo.
Baada ya muda  mwandishi alimtafuta  kamanda huyo lakini hakuweza kulizungumzia akisema alikuwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Uwanja wa Taifa, kwenye kikao na wanamichezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,603FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles