Safina Sarwatt Moshi,
KAMISHNA wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Liberatus Sabas amewaonya maofisa wa jeshi Polisi kuachana na matumizi ya nguvu kupitia kiasi na kuwabambikia watu kesi.
Kamishna Sabas alitoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya uongozi mdogo ndani ya jeshi la polisi ngazi ya koplo katika Shule ya Polisi Moshi Mkoani Kilimanjaro.
“Hakikisheni mnasimamia usalama wa wananchi na mali zao epukeni matumizi ya nguvu kupitia kiasia ,”alisema.
Alisema koplo ni cheo muhimu ndani ya jeshi hilo, hivyo nilazima waonyeshe nidhamu ya hali ya juu na kusisitiza ndio jambo muhimu katika utendaji kazi.
“Fanyeni kazi kwa ufanisi, epukeni vitendo vya rushwa nidhamu ni nguzo kuu ndani ya jeshi letu, ni wajibu askari kusimamia maadili, “alisema.
Alisema kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuimarishe ulinzi na usalama kwa vyama vyote siasa pamoja wapiga kura .
Mkufunzi Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi, Gemini Mushy alisema katika mafunzo hayo,wanafunzi walioripoti shule 1,016,kati wanafunzi 12 walishindwe kuendelea na mafunzo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo utovu wa nidhani,na maradhi.
“Wanafunzi 928 walimaliza mtihani,kati ya hao 896 ndiyo wamefaulu,50 wamefeli,huku wanafunzi 87 waliochelewa kuripoti shule hawakuweza kufanya mtihani na kwamba watabaki shule ili wamalize masomo ,”alisema.