22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Polisi waokoa watoto watano

mtoto kuuzwa

Jeshi la polisi mkoani Mara linamshikilia mwanamke mmoja, Juritha Lucas (60)wa Kijiji cha Masinki wilayani Serengeti kwa tuhuma za kufanya biashara haramu ya kuuza binadamu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Ramadhani Nganzi, mwanamke huyo alikamatwa  akiwa na mabinti watano aliokuwa anataka kuwauza ambao umri wao ni kati ya miaka 15 na 23 na wakazi wa Kijiji cha Muruvyagiza, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Dhumuni ni kuwaozesha kwa wanaume kwa Shilingi 150,000 hadi Sh 300,000, bei ambazo zinaendana na umri, uzuri na tabia

Mwanamke huyo yuko chini ya ulinzi na polisi bado wanaendelea na uchuguzi kujua mtandao wake kujua kama ana wakala mkoani Kagera ambaye amekuwa akimkusanyia mabinti hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles