21.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 5, 2022

Polisi wanasa watatu tuhuma kumnywesha mtoto bia

Mwandishi Wetu- Shinyanga

JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga, linawashikilia watu watatu kwa kosa la kumpeleka baa mtoto  wa kike mwenye umri wa miaka mitatu na kumnywesha bia aina ya Balimi.

Kibaya zaidi, watu hao wakati wakimwenyesha pombe, walikuwa wakimrekodi video, kisha kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,Debora Magiligimba alisema tukio hilo lilitokea Aprili 24,mwaka huu saa 6 mchana kwenye baa ya  Bondeni iliyopo Kijiji cha Nyaligongo. 

“Tunawashikilia watu watatu ambao ni Godius Katisha (32),mkazi wa Mwakitolyo ambaye ni baba wa mtoto, mmiliki wa baa,Irene Pima (32), mkazi wa Namba 2 Mwakitolyo na Oscar Daniel Makondo (35) mkazi wa Mtaa wa Mayila wilayani Kahama kwa makosa ya ukatili dhidi ya mtoto na matumizi mabaya ya mitandao. 

“Siku ya tukio mtoto wa kike, mwenye umri wa miaka mitatu, mkazi wa Mwakitolyo alifanyiwa ukatili kwa kupelekwa kwenye baa hiyo na kunyweshwa pombe aina ya Balimi na kurekodiwa video kwa kutumia simu, kisha kurushwa kwenye mitandao ya kijamii na kuonekana kwenye magroup ya whatsapp”,alisema. 

Alisema baada ya tukio hilo, kikosi kazi cha askari wa uhalifu wa makosa ya kimtandao waliwakamata watuhumiwa hao akiwemo baba mzazi wa mtoto, Godius Novat Katisha. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,680FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles