32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Polisi wanasa silaha za kivita Dar

Kamishina wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro.
Kamishina wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro.

NA TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,limesema limekamata bunduki 10 wakati wa operesheni ya kuwasaka watuhumiwa wanaodaiwa kuua askari wa jeshi hilo katika eneo la Mbande.

Watu wasiojulikana walivamia Benki ya CRDB Tawi la Mbande na kuwaua askari wanne,huku wakiwanyang’anya silaha walizokuwa nazo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini wake Dar es Salaam,Kamishina wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro alisema jeshi hilo liliendesha operesheni maeneo mbalimbali na kukamata wahalifu hao ambao hakutaka kutaja idadi yao ili kutoharibu ushahidi.

“Tumekamata bunduki za kivita saba na ndogo tatu ambazo walikutwa nazo watuhumiwa hao,” alisema Kamanda Sirro.

Alisema katika mahojiano na watuhumiwa hao, walikiri kufanya mauaji hayo huku wakidai shida yao kubwa ni kupata silaha tu.

Katika hatua nyingine, Kamanda Sirro alisema jeshi hilo linamshikilia mkazi wa Goba, Mussa Katela maarufu Ferali(36) kwa tuhuma za kujihusisha na ujambazi wa kutumia silaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles