23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Polisi wafunguka msaidizi wa Membe

 NASRA HUSSEIN Na SALOME BRUNO (TUDARCO)

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema msaidizi wa mgombea urais wa ACT Wazalendo, Bernard Membe anayedaiwa kutekwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Akizungumza jana wakati wa kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana katika Hospitali ya Polisi iliyopo Kurasini, alisema msaidizi huyo, Jerome Luanda anahojiwa kwa kosa la kutakatisha fedha.

Mambosasa alisema kuna watu wameanza kusambaza taarifa kuwa msaidizi huyo amekamatwa na watu wasiofahamika na kushauri kama mtu anahitaji taarifa kamili awasiliane na Jeshi la Polisi.

Luanda alidaiwa kutekwa hivi karibuni baada ya Membe kufika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam akitokea nchini Dubai.

 Juzi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Membe aliandika; “tukio la kutekwa kwa msaidizi wangu Jerome Luanda jana (Septemba 15) mara baada ya kutua kwenye kiwanja cha Kimataifa cha JK Nyerere international Airport nitalizungumzia kwa undani saa 10 kamili leo (jana). Nimewapa wahusika wanaodhani siwajui masaa matatu wamwachie akiwa mzima na salama.”

Baada ya jana taarifa ya Mambosasa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Membe tena kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika; “afande kama taarifa hii ni ya kweli, 1. Yupo (Jerome) kituo gani cha polisi na kwa tuhuma zipi ili sisi wanafamilia na wanasheria wetu tuende tukamwone? 2. Mbona amekaa polisi zaidi ya masaa 24 muda ambao kisheria alitakiwa awe amehojiwa na kupelekwa mahakamani au kuachiwa huru?”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,642FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles