27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi wafukuzana na majambazi mitaani

Leonard-PauloNa SUSSAN UHINGA, TANGA

WAKAZI wa jijini Tanga, jana walijikuta katika hofu kwa saa kadhaa baada ya askari polisi kufukuzana na majambazi mitaani kwa kutumia pikipiki na magari ya raia.

Wakati wa tukio hilo lililotokea jana asubuhi, majambazi hao walikuwa wakiendesha gari lao kwa mwendo kasi huku raia na askari polisi wakiwafuatilia kwa mwendo kasi pia, hali iliyosababisha wananchi kujawa na hofu huku shughuli za maendeleo zikisimama.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo, alisema majambazi hayo yalikuwa yakitumia gari aina ya toyota probox.

“Kabla ya tukio hilo, majambazi walikurupushwa kutoka kwenye maegesho ya magari ya Halmashauri ya Jiji, walitoka mbio na kuelekea Barabara ya Horohoro.

“Wananchi na waendesha bodaboda walipoona polisi wanawakimbiza, nao wakaungana na askari hao kuwakimbiza majambazi hao.

“Majambazi walipoona wanaweza kukamatwa wakiwa katika barabara hiyo, waligeuza haraka gari lao na kuelekea Barabara Kuu ya Tanga-Segera.

“Kwa kweli tukio hilo liliwashtua sana wananchi waliokuwa kando ya
barabara kwa sababu wengi wao walikuwa hawajui kinachoendelea kutokana na magari na pikipiki zilivyokuwa zikikimbia kwa kasi,” alisema Kamanda Paulo.

Pamoja na majambazi hayo kutaka kuwakwepa polisi, Kamanda Paulo alisema wawili kati ya majabazi wanne yaliuawa kwa kupigwa risasi baada ya kutaka kuwashambulia polisi.

“Hata hivyo, majambazi wawili waliokuwa na silaha, walifanikiwa kutoroka na kukimbilia katika msitu ulipo jirani na Kiwanda cha Sungura,” alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Paulo, majambazi hao ndiyo walimpora begi daktari kutoka Ujerumani aliyeko katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Anna Wandest.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles